KATIKA kuendeleza shughuli mbalimbali za kuinua Mkoa wa Mara na kuimarisha ustawi wa jamii, Mbunge Agnes Marwa ametunukiwa Tuzo ya Heshima na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Mara, kwa kutambua mchango wake wa hali na mali katika kuimarisha Jumuiya hiyo na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo. Tuzo hiyo imekabidhiwa na Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Godfrey Kavenga, akiambatana na viongozi wa UWT, ambaye amesema hatua hiyo inalenga kutambua jitihada, kujitolea na ushirikiano wa Agnes Marwa katika kuendeleza shughuli za Jumuiya na kugusa maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali. Kavenga amesema mchango wa Agnes Marwa umeonekana katika shughuli mbalimbali zinazolenga kuimarisha Jumuiya ya UWT Mkoa wa Mara, huku akimtaka kuendelea na moyo huo wa kujitolea na kushirikiana na wanawake pamoja na jamii katika kuleta maendeleo. Kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika kata ya MWISENGE Mh Agnes Marwa alifanya ziara na shughuli za kijamii katika Wil...
Marato tv - Sauti ya Jamii