Kufuatia taarifa iliyochapishwa na chombo kimoja cha habari na kusambaa katika mitandao ya kijamii, ikidai kuwa walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wameagizwa kuendelea kufundisha hadi Desemba 20, uchunguzi uliofanywa na George Marato TV umebaini kuwa taarifa hiyo si sahihi na haioneshi uhalisia wa utaratibu unaotekelezwa katika halmashauri hiyo. Uchunguzi umebaini kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba haiendelezi shughuli za ufundishaji wakati wa likizo za shule, isipokuwa wanafunzi hupangiwa zamu maalumu za kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira ya shule pamoja na kuhudumia mashamba ya shule yanayozalisha chakula kwa ajili ya matumizi yao. Aidha, taarifa iliyochapishwa na chombo hicho cha habari ilidai kuwa mdau mmoja wa elimu alikuwa ameitaka Idara ya Elimu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kuingilia kati agizo hilo linalodaiwa kutolewa, kuchunguza utaratibu wa malipo ya walimu na kuhakikisha walimu pamoja na wanafunzi wanapata likizo kwa mujibu wa miongozo iliy...
Marato tv - Sauti ya Jamii