Skip to main content

Posts

Showing posts from November 8, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUANZIA UTOTONI YATAJWA SILAHA YA KUPUNGUZA AJALI

Kuwafundisha watoto matumizi sahihi ya barabara wakiwa katika umri mdogo inatajwa kuwa hatua muhimu inayoweza kusaidia kujenga kizazi chenye nidhamu ya kuzingatia sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika. Hayo yameelezwa na Afisa kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dodoma kitengo cha elimu SGT Ester Makali, wakati akizungumza na washiriki wa programu ya VIA – Global Road Safety Education via a New Generation, iliyolenga kuwajengea watoto na vijana uelewa kuhusu matumizi salama ya barabara. SGT Makali amesema elimu hiyo inapaswa kuanza mapema ili watoto waweze kujenga mazoea sahihi wanapotumia barabara, ikiwemo kujua namna salama ya kuvuka, kutambua alama za barabarani na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha yao. "Kuwajengea watoto uelewa huo tangu wakiwa wadogo kunaweza kuwasaidia kuwa watumiaji wa barabara wanaowajibika wanapokua pamoja na kuifikisha elimu hiyo kwa familia na jamii zinazowazunguka,"amesema. Kwa upande wao, wanaf...

AGNESS MARWA ATOA MSAADA WA SARUJI,MISWALA NA JUZUU ZA KUJIFUNZIA MSIKITI WA IR

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Agness Marwa, ameendelea kuonesha mfano wa mshikamano na upendo katika jamii kwa kushiriki ibada katika Msikiti wa Iringo, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, na kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi pamoja na mahitaji ya ibada na kujifunzia. Katika ziara hiyo, Mbunge huyo amekabidhi mifuko mitano ya saruji, juzuu za kujifunzia pamoja na miswala ya kuswalia, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuchangia maendeleo ya taasisi za kidini na kuimarisha mahusiano baina ya waumini wa dini mbalimbali. Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Sheikh Amani Kapama wa Msikiti wa Iringo, amempongeza Mheshimiwa Marwa kwa moyo wake wa kujitolea na utaratibu wake wa kutembelea na kusaidia taasisi za kidini, akisema hatua hiyo imekuwa daraja muhimu la kuunganisha jamii bila kujali tofauti za kiimani. Amesema ushirikiano unaooneshwa na Mbunge huyo unachangia kujenga mshikamano baina ya Waislamu na wasio Waislamu, kuimarisha upendo na kuendeleza misingi ya umoja na a...

MAVUNDE:STAMICO IMARISHENI UWEKEZAJI NA UZALISHAJI WA NISHATI SAFI

 WAZIRI wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuimarisha uwekezaji na uzalishaji ili ndani ya miaka mitatu liweze kufikia kiwango cha kushindana na kampuni kubwa za uchimbaji madini nchini, zikiwemo Barrick, Geita Gold Mine na Shanta. Mavunde ametoa changamoto hiyo Novemba 7, 2026, wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Nishati Safi cha Rafiki Briquettes kilichopo Chigongwe, mkoani Dodoma, akieleza kuwa STAMICO ina rasilimali na fursa nyingi zinazopaswa kutumiwa kuifanya kuwa taasisi imara na yenye mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Amesema STAMICO imepiga hatua kubwa katika kuimarisha utendaji wake, ikilinganishwa na hali ya miaka mitano iliyopita ambapo shirika hilo lilikuwa katika changamoto za kifedha na kutegemea ruzuku ya Serikali. Kwa mujibu wa Mavunde, mapato ya shirika yameongezeka kutoka Shilingi bilioni moja hadi zaidi ya Shilingi bilioni 89 chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Venance Mwasse. Ameeleza kuwa shirika hilo l...