Serikali imeendelea kuimarisha juhudi za kuboresha ubora wa elimu nchini kwa kuhamasisha ubunifu na umahiri wa walimu, ambapo walimu 3,153 wamejisajili kushiriki Shindano la Taifa la Stadi za Ufundishaji la mwaka 2026, linalolenga kuibua mbinu bunifu za ufundishaji na kujifunzia ili kuongeza matokeo bora ya elimu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelekea hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Afidhi Ameir, amesema shindano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mageuzi ya sekta ya elimu pamoja na Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa elimu ya awali na wanafunzi wa madarasa ya chini. Amesema serikali inalichukulia shindano hilo kama jukwaa muhimu la kuwapa walimu nafasi ya kuonesha uwezo wao, kubadilishana uzoefu na kuibua mbinu mpya zinazoweza kuimarisha ufundishaji darasani. "Shindano hili linatoa fursa kwa walimu kuonesha umahiri wao, kuba...
Marato tv - Sauti ya Jamii