Skip to main content

Posts

Showing posts from July 28, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS SAMIA AONGOZA KAMATI KUU YA CCM ZANZIBAR

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao Cha Kamati Kuu ya Halamshauri Kuu ya CCM Taifa tarehe 29 Julai 2026 Zanzibar

MARY SURATI ACHAGULIWA KUNDI LA KWANZA LA WANAWAKE VIONGOZI AFRIKA

 MBUNGE wa Jimbo la Serengeti, Mhe. Mary Daniel Surati (MB), amepata heshima kubwa baada ya kuchaguliwa kuwa miongoni mwa washiriki 40 wa kundi la kwanza la waanzilishi (Founding Fellows) wa programu ya African Academy for Women in Political Leadership, inayotekelezwa kupitia African School of Governance (ASG). Uteuzi huo umefanyika baada ya mchakato wa ushindani uliowashirikisha waombaji 1,334 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, jambo linaloonyesha kiwango cha juu cha ushindani na ubora wa washiriki waliochaguliwa kujiunga na programu hiyo ya kimataifa inayolenga kuwaandaa wanawake viongozi wa kizazi kipya barani Afrika. Akizungumzia mafanikio hayo, Mhe. Surati amesema anajivunia kuwa sehemu ya kundi la kwanza la waanzilishi wa programu hiyo, akieleza kuwa ni fursa muhimu ya kujifunza, kukuza uwezo wake wa uongozi na kujenga mtandao wa ushirikiano na wanawake viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Amesema mafunzo hayo yatamwezesha kupata maarifa mapya kuhusu uongozi wa kisias...

DR. JUDITH MHINA RAISES THE TANZANIAN FLAG HIGH IN CHINA

 By Staff Writer A leading Tanzanian businesswoman in the port and maritime transport sector, Dr. Judith Mhina Spendi, continues to represent Tanzania on the international stage following her participation in a major conference on Indian Ocean shipping held in Zhoushan, China. The high-level forum brought together shipping executives, port authorities, investors, and policymakers from across Asia, Africa, and the Middle East to discuss the future of maritime trade in the Indian Ocean region. Dr. Judith’s invitation to the conference underscores the recognition Tanzania is receiving as a key player in East Africa’s blue economy. Dr. Judith is among the few Tanzanian women who have successfully established a strong presence in the maritime shipping sector through PMM Group. The company has built a solid reputation in cargo shipping across the Indian Ocean, inland container depot management, and operations linked to the mining and environmental sectors. Over the years, PMM Group has p...

SEKTA BINAFSI YATAJWA NGUZO MUHIMU KUFANIKISHA DIRA YA TAIFA 2050

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema sekta binafsi ina nafasi ya kipekee katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku akiwataka viongozi na watumishi wa umma kubadili mtazamo na kuiona kama mshirika muhimu wa maendeleo badala ya mpinzani. Akifunga kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Mkoa wa Dodoma kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Senyamule alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita katika kujenga uchumi unaomilikiwa na Watanzania kupitia uwekezaji wa ndani na ushirikiano imara kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. "Katika kutekeleza Dira ya Taifa 2050, tutaendelea kupokea wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Wawekezaji kutoka nje watakuja na mtaji na teknolojia, huku Watanzania wakinufaika kupitia ajira, mapato ya kodi na ukuaji wa uchumi. Hivyo, ni muhimu tubadili mtazamo wetu na kuitambua sekta binafsi kama mshirika wetu wa maendeleo," amesema...

DKT. JUDITH MHINA SPENDI AIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWENYE JUKWAA LA KIMATAIFA LA UCHUMI WA BAHARI CHINA

 Zhoushan, China.  Mfanyabiashara mashuhuri wa Kitanzania na Mkurugenzi wa PMM Group, Dkt. Judith Mhina Spendi, ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa baada ya kushiriki mkutano wa kibiashara katika sekta meli   unaowakutanisha viongozi, wawekezaji na wadau wa sekta ya bandari, uchukuzi na usafirishaji wa baharini kutoka mataifa mbalimbali, uliofanyika  Shipyard Jijini Zhoushan Nchini China.  Ushiriki wa Dkt. Judith katika mkutano huo unaashiria kuongezeka kwa nafasi ya Watanzania, hususan wanawake, katika majukwaa ya kimataifa yanayojadili mustakabali wa biashara ya baharini, uchumi wa buluu na maendeleo ya sekta ya usafirishaji duniani. Dkt. Judith ni miongoni mwa wanawake wachache nchini Tanzania waliofanikiwa kujenga na kuongoza kampuni kubwa inayotoa huduma za ugavi na usafirishaji wa mizigo kupitia bahari.  Kupitia PMM Group, kampuni hiyo imejipambanua katika huduma za usafirishaji wa mizigo katika Bahari ya Hindi, usimamizi wa ba...

TANESCO: BAADHI YA MIKOA KUKOSA UMEME KWA MUDA KUPISHA UKAMILISHAJI WA MRADI WA 400KV CHALINZE–DODOMA

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuwa baadhi ya mikoa nchini itakumbwa na kukosekana kwa huduma ya umeme kwa muda katika kipindi cha kuanzia Julai 30 hadi Agosti 17, 2026, ili kupisha utekelezaji wa hatua za mwisho za Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma. Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Irene Gowele, amesema mradi huo umefikia asilimia 94 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika rasmi Agosti 21, 2026. Amesema hatua zilizobaki zinahusisha kazi ya kuvuta nyaya za umeme katika maeneo ya Mkambalani mkoani Morogoro na Kikombo mkoani Dodoma, kazi inayohitaji baadhi ya njia za kusafirisha umeme kuzimwa kwa muda ili kuhakikisha usalama wa wafanyakazi, wananchi pamoja na miundombinu ya umeme wakati wa utekelezaji wa mradi huo. "Kazi hizi ni muhimu kwa ajili ya kukamilisha mradi huu wa kimkakati, hivyo kutakuwa na ulazima wa kusitisha huduma ya umeme katika...

SSP SODOKA: VIJANA WAWE MSTARI WA MBELE KULINDA AMANI

  Na Dawati la Habari Polisi Mwanza Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyamagana limewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani na usalama wa jamii kwa kushirikiana kwa karibu na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na serikali za mitaa katika kuwabaini na kuwafichua wahalifu wanaojificha kwenye maeneo yao. Wito huo umetolewa Julai 26, 2026 na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, SSP Virginia Sodoka, wakati wa fainali za mashindano ya Polisi Jamii Cup zilizofanyika katika Kata ya Mirongo, ambapo Mashi FC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Mirongo FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mirongo. Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi na mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia fainali hizo, SSP Sodoka alisema vijana ni nguvu kazi ya taifa na nguzo muhimu katika kuhakikisha mfumo wa Polisi Jamii unafanikiwa. "Vijana wana nafasi kubwa ya kuwa walinzi wa amani katika jamii. Mkiamua kushirikiana na Jeshi la Polisi mtasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea. Lakini pia msipo...

POLISI, TRC WAHAMASISHA WANANCHI KULINDA MIUNDOMBINU YA RELI

Wananchi wa Kata ya Mwabomba, hususan Kijiji cha Mhulula wilayani Kwimba, mkoani Mwanza, wamehimizwa kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu ya reli kwa kutambua kuwa uwekezaji huo ni mali ya Watanzania wote na una mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa. Rai hiyo imetolewa Julai 27, 2026 na Mkuu wa Kituo cha Polisi Reli Mkoa wa Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliowakutanisha viongozi wa serikali za vijiji na kata, wataalamu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na Jeshi la Polisi. Mkutano huo ulilenga kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya reli, usalama wa jamii, kuzuia ukatili wa kijinsia na utatuzi wa migogoro ya ardhi. Akizungumza na wananchi, Mkuu wa Kituo cha Polisi Reli Mkoa wa Mwanza, ASP Jovitha Tibangayuka, alisema ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya jamii na Jeshi la Polisi katika kulinda miundombinu ya reli na rasilimali nyingine za taifa. "Jukumu la kulinda miundombinu ya reli ni la kila mwananchi. Si la Kikosi cha Polisi Reli au Shirika ...