Skip to main content

Posts

Showing posts from August 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MARA YAJIPANGA KUNUFAIKA NA FURSA ZA KONGAMANO LA TAIFA LA KILIMO MISITU

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Kanali Evans Alfred Mtambi, leo tarehe 21 Agosti 2026, amewapokea na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Vi Agroforestry kuhusu maandalizi ya Kongamano la 11 la Taifa la Kilimo Misitu, litakalofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Oktoba 2026 katika Kituo cha Mafunzo cha Agroforestry (ATC), Bweri, Manispaa ya Musoma. Mazungumzo hayo yalijikita katika maandalizi ya kongamano hilo, ambalo linalenga kuhamasisha kilimo misitu kama nyenzo ya kuongeza uzalishaji, kuhifadhi mazingira, kuimarisha usalama wa chakula na kuinua uchumi wa wananchi. Akizungumza katika kikao hicho, Mheshimiwa Kanali Mtambi amewashukuru Vi Agroforestry kwa juhudi wanazozifanya kila msimu katika kuhakikisha vijana na Watanzania kwa ujumla wanaelewa fursa zilizopo katika sekta ya kilimo.  Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mara, hususan vijana, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo ili kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuibua wigo mpya wa fursa za maendeleo ya k...

MASWI, DKT. KIDA WAJADILI UFUNGAMANISHAJI JAMII AJENDA NA DIRA 2050

 Katibu Mkuu @maendeleoyajamii, Eliakimu Maswi na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi M. Kida, leo Agosti 20, 2026 wamejadiliana kuhusu ufungamanishaji wa Ajenda ya Kitaifa ya Mageuzi ya Kijamii na Maendeleo ya Mtaji Watu katika Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Dira 2050. Majadiliano yao yamejikita katika umuhimu wa kuhakikisha mipango na mikakati ya kisekta hususani sekta ya maendeleo ya Jamii, inaendana na vipaumbele vya Taifa vilivyowekwa katika Dira 2050 na mipango ya maendeleo ya muda mrefu na muda wa kati, ili iweze kutoa mchango unaopimika katika kufikia malengo ya Taifa. Dkt. Kida amesema baada ya Dira 2050 kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Julai 17, 2025, na kuzinduliwa kwa nyenzo za utekelezaji wake Agosti 3, 2026, ni muhimu kila taasisi na mdau kuhakikisha mikakati na programu zake zinafungamana na malengo ya Dira hiyo. “Nikupongeze Katibu Mkuu Maswi kwa kuchukua hatua ya kuoanisha m...

WAZIRI OMAR ASHUKURU IMF KWA USHIRIKIANO WA MUDA MREFU NA TANZANIA

 Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, amelishukuru Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa mchango wake kwa Tanzania tangu kuanza kwa ushirikiano kati yake na Shirika hilo, akieleza kuwa ushirikiano huo umeendelea kuwa muhimu katika kuimarisha uchumi na utekelezaji wa ajenda za maendeleo nchini. Ametoa Shukran hizo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi mpya wa IMF nchini Tanzania, Bi. Jana Bricco, ambaye ameanza rasmi majukumu yake nchini, ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Tanzania na IMF, ambao umedumu kwa zaidi ya miongo sita tangu uanzishwe miaka ya 1960. Mhe. Balozi Omar amesema Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na IMF katika kufanikisha ajenda ya maendeleo ya Tanzania, ikiwemo utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na mwelekeo wa kimkakati wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaofuata ambayo ni maeneo yenye manufaa kwa pande zote na yanayochangia utekeleza...

RAIS SAMIA KUWAREJESHA NYUMBANI WATANZANIA 669 KUTOKA AFRIKA KUSINI

 WATANZANIA 669 waliopo Afrika Kusini wanatarajiwa kurejea nchini kwa hiari yao kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwawezesha kurejea nyumbani na kuungana na familia zao. Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana, ameyasema hayo leo kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza na kundi la kwanza la Watanzania 241 kutoka Durban, Jimbo la KwaZulu-Natal, watakaorejea nchini Agosti 26, 2026 kwa ndege ya Air Tanzania. Kwa mujibu wa Balozi Bwana, Watanzania hao watafanyiwa uhakiki Agosti 25 na 26 kwa kushirikisha Ubalozi wa Tanzania na mamlaka za Afrika Kusini, kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini. Amesema mpango huo umeanza baada ya Watanzania hao kuomba kwa hiari yao msaada wa Serikali ili waweze kurejea Tanzania, baada ya kuishi Afrika Kusini kwa muda mrefu. “Mheshimiwa Rais amewakaribisha tena nyumbani na amenielekeza kama Balozi wake hapa Afrika Kusini kuhakikisha Watanzania walio tayari kurejea...

DKT. MWIGULU ATOA MAELEKEZO VIWANJA VYA AFCON

▪︎ Ataka kazi ifanyike usiku na mchana inapowezekana ▪︎ Asisitiza mashindano hayo ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa Tanzania WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kuongezwa kasi ya ujenzi wa viwanja vya mazoezi vitakavyotumika katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ili vikamilike kwa wakati na kukidhi viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Amesema kazi hiyo inapaswa kufanyika kwa kasi, ikiwemo kuongeza muda wa kufanya kazi pale inapobidi, ili viwanja vikamilike kwa wakati na Tanzania iwe tayari kabla ya ukaguzi wa maandalizi unaotarajiwa kufanywa na CAF. Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo (Ijumaa, Agosti 21, 2026) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa viwanja vya mazoezi vya Farasi na Leaders Club jijini Dar es Salaam, ambavyo ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika katika maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027 yatakayofanyika kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda. Amesema Tanzania haipaswi kusubiri hadi dakika za mwisho...

DC CHIKOKA AWAKUMBUSHA WAJUMBE WA KAMATI YA AFYA MSINGI (PHC)KUFANYA KAZI KWA UFANISI KUELEKEA ZOEZI LA UTOAJI CHANJO YA POLIO

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano MKUU wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara Juma Chikoka awakumbusha wajumbe wa kamati ya Afya ya msingi(PHC) Kufanya kazi kwa ufanisi kuelekea zoezi la chanjo ya Polio ya matone(nOPV2) linalitarajia kufanyika Agosti 27-30. Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wajumbe hao katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma ikiwahusisha washiriki kutoka halmashauri ya Musoma vijijini na halmashauri Manispaa ya Musoma. Chikoka amesema kuwa katika halmashauri ya Musoma vijijini wanatarajia kuwafikia watoto walio chini ya miaka 10 wapatao 118,936 huku halmashauri ya Manispaa ya Musoma inatarajia kuwafikia watoto wapatao 66,176. Amesema atahakikisha hamasa na elimu ya kutosha itatolewa kwa jamii ili kuwajengea uelewa wa kutosha kuhusu chanjo hii ambayo inakwenda kuondoa changamoto ya ulemavu kwa watoto. "Tutaendelea kufanya ushirikishwaji na kushirikiana ili kuleta mapokeo na matokeo makubwa na kila mmoja atimize wajibu wake,"amesema Chikoka. Ili kufikia ma...

MWANAFUNZI WA AMALI AONESHA UMAHIRI KATIKA KUCHAMBUA MFUMO WA INJINI YA GARI

Wakati Maonesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yakiendelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga, mwanafunzi wa mkondo wa Amali kutoka Shule ya Sekondari Tanga Ufundi, Neema Bundara (16) ameonesha umahiri wa kuchambua na kuelezea mfumo mzima wa injini ya gari. Akionesha umahiri huo leo Agosti 21,2026 mwanafunzi huyo wa kidato cha Tatu ametumia mfano wa injini kuonesha kazi za sehemu mbalimbali zinazounda mfumo wa injini, akieleza namna kila kifaa kinavyoshirikiana kuzalisha nguvu ya kuendesha gari. Katika maelezo yake amesema cylinder block, pistoni na connecting rod hufanya kazi kwa pamoja kuruhusu pistoni kusogea juu na chini, hatua inayowezesha mzunguko wa mwako ndani ya injini. "Crankshaft na camshaft huunganishwa na timing chain ili kuratibu mzunguko wa injini na kuhakikisha vali zinafunguka na kufunga kwa wakati sahihi,"ameeleza. Aidha, akielezea mfumo wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira, amesema catalytic converter, muffler na tail pipe husai...

WORLDSKILLS TANZANIA, ENABEL YAONGEZA NGUVU KWA VIJANA WENYE VIPAJI

Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (Enabel) limesema litaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha vijana wanaoshiriki Mashindano ya Kitaifa ya Ujuzi WorldSkills Tanzania 2026 wanapata fursa za ajira na kufikia ushindani wa kimataifa. Akizungumza leo Agosti 21,2026 katika maonesho ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika viwanja vya shule ya sekondari Usagara jijini Tanga Mwakilishi wa Enabel nchini, Abel Mbilinyi amesema shirika hilo ni miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo kwa kutoa vifaa vya mashindano, zawadi kwa washindi na kumleta mtaalamu kutoka Ubelgiji kwa ajili ya kujenga uwezo wa waandaaji na majaji. Mbilinyi amesema Enabel imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuwawezesha vijana kupata ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira kupitia ushirikiano na taasisi za mafunzo ya ufundi ikiwemo VETA na taasisi nyingine za elimu ya ujuzi. "Lengo kuu la shirika letu ni kuhakikisha vijana wanapata ajira za staha, huku wengine wakipewa uwezo wa kuj...

WAZIRI MAVUNDE AKUTANA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI

 Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde leo tarehe 21.08.2026 Jijini Dodoma amekutana na kujadiliana na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Saudi Gold Refinery Ndg. Faisal Alothaim juu ya mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya Madini nchini Tanzania. Mh. Mavunde amewahakikishia wawekezaji hao kwamba serikalinya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini Tanzania na uwepo wa madini mengi nchini Tanzania unatoa fursa kwa wigo mpana wa eneo la uwekezaji. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Saudi Gold Refinery Ndg. Faisal Alothaim ameshukuru Tanzania kwa maandalizi mazuri ya Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Saud Arabia ambalo limefungua fursa kubwa ya ushirikiano kupitia nchi hizi mbili. Ameongeza kwamba,Tanzania ni kati ya nchi zenye mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba Kampuni yake ipo tayari kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Madini kwa kufanya utafiti wa kina na baadaye uwekezaji mkubwa wa u uchimbaji wa...