Skip to main content

Posts

Showing posts from October 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WADAU WAIPONGEZA THBUB KUFANYA UTAFITI KUHUSU UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Baadhi ya Asasi za Kiraia zimeipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kufanya utafiti kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Mkoa wa Arusha. Pongezi hizo zimetolewa na wawakilishi wa asasi hizo wakati wa majadiliano na THBUB yaliyolenga kukusanya taarifa za l utafiti kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani humo. Akizungumza Oktoba 21, 2026 wakati wa majadiliano yaliyofanyika katika ukumbi wa Center For Women and Children Development,Jijini Arusha. Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake na Watoto Bi.Hindu Mbwego amesema kuwa anapata faraja kuona THBUB ikitekeleza jukumu lake la kikatiba la kufanya tafiti zinazohusu masuala ya haki za binadamu. Bi. Hindu amesisitiza kuwa utafiti huo ni muhimu katika kubaini hali halisi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, changamoto zinazowakabili waathirika pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa na wadau mbalimbali katika kukabiliana na tatizo hilo. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu...

JUHUDI ZA UPANDAJI MITI ZIONGEZWE MKOANI KIGOMA.

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Mkoa Kigoma umekuwa ukipokea wakimbizi wengi kwa miaka mingi kumekuwa na utumiaji mwingi wa nishati ya kuni hali iliyopelekea uharibifu wa mazingira. Mara baada ya kupata maelezo mafupi katika banda la Vi Agroforestry kutoka kwa Afisa ufuatiliaji na tathmini Stella Msami kuwa hivi sasa kuna mradi wa miaka mitatu utakaopelekea vijana wengi kujifunza hivyo amemtaka mgeni rasmi kupendekeza mkoa ambao utakuwa ni mmojawapo wa wanufaika wa mradi huo. Amesema Stella kutokana na uwepo wa mradi huo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi tutajitahidi kufikisha ujumbe wa upandaji miti kwa mkoa pendekezwa ukizingatia kwamba upandaji miti ndio nguzo pekee itakayosaidia kukabili mabadiliko ya tabia nchi. Kwa Upande wake Katibu Tawala mkoa wa Mara Gerald Musabila Kusaya amelitaka shirika la Vi Agroforestry kuongeza juhudi za upandaji miti Mkoa wa Kigoma kutokana na uwepo wa historia ya matumizi makubwa kuni. " Tunakwenda kupanda miti kule Kigoma kwa sab...

BIDHAA NYINGI ZAZALISHWA KUPITIA KILIMOMISITU.

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. Katika kuhakikisha Dira ya maendeleo ya 2050 inafanikiwa na kila mwananchi kuishiriki vema kuna umuhimu mkubwa wa kuhamasisha Kilimomisitu. Katika kongamano la  Kitaifa la kumi na moja la Kilimo Misitu ambalo limelenga kuimarisha mazingira ya kisera yenye ustahimilivu kwa maendeleo ya kilimo nchini limeendelea kuwezesha fursa ya ajira kwa makundi mbalimbali hapa nchini. Bidhaa nyingi zimeletwa na  makundi mbalimbali yanayojihusisha na kilimo,ufugaji na usindikaji. Mtandao wa Vikundi vya wakulima na wafugaji Nyancha( MVIWANYA) ni miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo ambao wameweza kuleta bidhaa mbalimbali. Mratibu wa Shirika la MVIWANYA  Joel Nguvava amesema makongamano kama haya yanawajengea uwezo wakulima na wafugaji  pia na kubadilishana uzoefu kupitia mafunzo mbalimbali yanayopelekea kuboresha shughuli zao. "Tunapata fursa ya masoko na wateja wapya na kutuwezesha kuongeza kipato na ajira kwa vijana",amesema Nguvav...

MSIMAMO WA TRA KUTOFUNGIA BIASHARA UMEZINGATIA MASLAHI YA PANDE ZOTE

NA: DK. REUBENI LUMBAGALA  Kuna mabadiliko makubwa ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa namna wanavyoendesha shughuli zao. Mabadiliko hayo yamezingatia kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi bila kuumiza upande mwingine. TRA katika kutimiza wajibu wake wa kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara na walipakodi wengine, wamebadili utaratibu wao wa awali ambao ulihusisha kufungia biashara kwa mfanyabiashara aliyeshindwa kulipa kodi kwa wakati. Jambo hili lilikuwa likilalamikiwa na walipakodi wengi kwani kufungia biashara kuliwaua kiuchumi wafanyabiashara na kufifisha matumaini ya kulipa kodi wanayodaiwa na TRA, hivyo serikali kukosa mapato yake. Kiufupi, utaratibu huu ulikuwa msiba mkubwa wa kiuchumi na maendeleo. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika maelekezo yake kwa TRA, alipiga marufuku matumizi ya vikosi kazi katika ukusanyaji kodi na kufungia biashara. Maelekezo hayo yakapokelewa vyema na TRA wakiongozwa na Kamishna Mkuu wake, CPA Yusuph Mwenda. Sasa ni faraja kuona kuwa, ...