Na Wellu Mtaki, Geita Benki ya Azania imeweka mkakati wa kuimarisha na kuongeza tija katika sekta ya madini nchini kwa kuwawezesha wadau mbalimbali wa sekta hiyo kupata mikopo yenye masharti rafiki, inayolenga kukidhi mahitaji ya kifedha katika hatua tofauti za mnyororo wa thamani wa madini, kuanzia wachimbaji wadogo hadi wawekezaji wakubwa. Kwa mujibu wa benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Tisa ya Madini Geita, imeeleza kuwa inatoa mikopo ya mitaji inayolipwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu kwa ajili ya kuendesha na kukuza biashara. Pia, benki hiyo inatoa mikopo ya uwekezaji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayohusiana na shughuli za uzalishaji. Mbali na mikopo hiyo, Benki ya Azania inatoa pia mikopo kwa ajili ya ununuzi wa mitambo na vifaa vya uzalishaji, ikiwemo mashine mbalimbali za viwandani pamoja na vifaa vinavyoweza kutumika katika shughuli za kutengeneza bidhaa kama betri. Aidha, benki hiyo imeeleza kuwa inawezesha wadau wa sekta ya madini kupata mik...
Marato tv - Sauti ya Jamii