Skip to main content

Posts

Showing posts from May 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kashfa za Ufisadi zamwandama Spika wa Bunge la Uganda Anita Anet Among

 Kwa miezi kadhaa sasa, siasa za Uganda zimeendelea kutikiswa na wimbi la tuhuma, uchunguzi wa kifedha na vita ya chini kwa chini ya kuwania madaraka ndani ya Bunge la taifa hilo, huku jina la Spika Anita Among likiendelea kutawala mijadala ya kisiasa nchini humo. Among, ambaye kwa muda mrefu alionekana kuwa mmoja wa wanasiasa wenye nguvu kubwa ndani ya utawala wa Rais Yoweri Museveni, sasa anakabiliwa na presha kubwa kisiasa kufuatia tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma pamoja na uchunguzi unaodaiwa kuwagusa baadhi ya viongozi waandamizi serikalini. Kupanda kwake kisiasa kulikuwa kwa kasi kubwa. Baada ya kifo cha aliyekuwa Spika Jacob Oulanyah mwaka 2022, Anita Among alichaguliwa kuongoza Bunge na haraka akajijengea ushawishi mkubwa ndani ya chama tawala cha NRM pamoja na miongoni mwa wabunge.  Uwezo wake wa kusimamia mijadala ya Bunge kwa msimamo mkali ulimfanya kuwa mmoja wa watu muhimu zaidi ndani ya mfumo wa utawala wa Museveni. Lakini nyuma ya nguvu hiyo y...

Rais wa Senegal Avunja Serikali Kufuatia Mvutano wa Kisiasa

 Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amemfuta kazi Waziri Mkuu Ousmane Sonko na kuvunja rasmi serikali yote kufuatia mvutano wa muda mrefu uliokuwa ukiendelea ndani ya uongozi wa nchi hiyo. Hatua hiyo ilitangazwa kupitia televisheni ya taifa usiku wa kuamkia leo, ambapo Ikulu ya Senegal ilieleza kuwa mawaziri wote wameondolewa madarakani huku serikali mpya ikitarajiwa kuundwa katika siku zijazo.  Serikali iliyovunjwa itaendelea kufanya kazi za kawaida za kila siku kwa muda mfupi hadi utawala mpya utakapotangazwa rasmi. Tukio hilo limewashangaza wananchi wengi wa Senegal pamoja na jumuiya ya kimataifa, hasa kutokana na ukweli kwamba Faye na Sonko walionekana kuwa washirika wa karibu kisiasa walioingia madarakani pamoja baada ya ushindi mkubwa wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.  Ushindi wao ulipewa taswira ya “mapinduzi ya kisiasa” yaliyomaliza utawala wa muda mrefu wa mfumo wa kisiasa uliokuwa ukitawala nchini humo kwa miaka mingi. Katika uchaguzi huo, Sonko alikuwa mwanasi...

Tawa Yawafikia Waganga wa Tiba Asili na Mbadala Kanda ya Ziwa

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Kituo Cha Mwanza imekutana na waganga wa tiba za asili na mbadala kwa kuwapatia elimu ya uhifadhi ikiwemo umiliki nyara wanazotumia katika shughuli zao. Akitoa elimu hiyo mbele ya Katibu Mtendaji wa Umoja wa Machifu Tanzania ambae pia ni  Mtemi Nyamilonda wa tatu Harun Mkomangwa  Wilayani  Ilemela mkoani humo mhifadhi wa wanyamapori kutoka TAWA Bw. Omary Mhando amewafafanulia umuhimu wa kutunza maliasili na kufuata taratibu za umiliki wa nyara kwa mujibu wa sheria za uhifadhi. Hakusita kuwambusha namna Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inavyoendelea kuwajali na kuwasikiliza wananchi wake na kutambua umuhimu wao na kuhakikisha inawajengea uelewa mpana kwa kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya uhifadhi ambayo itawezesha kuongeza wigo mpana wa kulinda maliasili kwa uhifadhi endelevu wenye misingi thabiti kwa vizazi hata vijavyo. Sanjari na hayo amewaeleza pia umuhimu ...

Jwtz na Majeshi ya EAC Yaimarisha Ushirikiano wa Kiusalama

Na Aron Msigwa, Nairobi – Kenya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Majeshi ya Ulinzi ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yamehitimisha kwa mafanikio zoezi la 14 la pamoja la Vituo vya Uamrishaji vya Kijeshi lijulikanalo kama Ushirikiano Imara 2026 jijini Nairobi, Kenya. Hafla ya kufunga zoezi hilo imehudhuriwa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Salum Haji Othman, aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda. Zoezi hilo kubwa la kijeshi limewakutanisha washiriki zaidi ya 400 kutoka Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda, Sudan Kusini, Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, likiwa na lengo la kuimarisha utayari, mshikamano na uwezo wa vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi wanachama wa EAC katika kukabiliana na changamoto na matishio ya kiusalama yanayolikabili eneo la Afrika Mashariki. Akizungumza wakati wa kufunga zoezi hilo, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya ...

Makaa ya Mawe ya Ruvuma Yafungua Masoko ya Afrika na Asia

Ruvuma Mkoa wa Ruvuma umeendelea kujizolea umaarufu katika sekta ya madini baada ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika wilaya za Mbinga, Songea na Nyasa kufungua masoko katika nchi mbalimbali za Afrika na Asia, huku zaidi ya tani milioni 3.6 zikizalishwa mwaka 2024/2025 na kuchochea ajira, biashara na matumizi ya nishati safi. Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi amesema shughuli za utafiti, uchimbaji na uchakataji wa makaa ya mawe zinazofanywa na makampuni pamoja na wadau mbalimbali zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla. Amesema makaa hayo yenye ubora wa hali ya juu yanatumika katika viwanda vya saruji, usafishaji wa vyuma na shughuli nyingine za viwandani, huku sehemu ya uzalishaji ikipelekwa katika masoko ya Kenya, Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). “Migodi ya makaa ya mawe ya Ruvuma imeendelea kuvutia wawekezaji kutokana na ubora wa madini hayo, hali iliyosaidia kufungua masoko mapy...

Ridhiwani Kikwete Aongoza Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa Bajeti ya EAC

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, leo Mei 22, 2026 jijini Arusha ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkutano huo ni hatua muhimu ya maandalizi ya Bajeti ya Jumuiya hiyo kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa ajili ya kujadiliwa na kuidhinishwa kabla ya Juni 30, 2026. Katika mkutano huo, Mhe. Ridhiwani Kikwete aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Cde. James Millya; Naibu Waziri wa Fedha Cde. Mshamu Ali Munde; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa; pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Serikali. Aidha, katika Mkutano huo wamejadili mipango ya kibajeti ya Taasisi mbalimbali ikiwemo Mahakama ya Haki ...

Rea washiriki mbio za Mwenge Wanging’ombe, yasambaza mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku

📍 *Wanging’ombe, Njombe* Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeshiriki katika sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 zilizofanyika Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, ambapo umesambaza na kuuza mitungi ya gesi ya kilo sita kwa wananchi kwa bei ya ruzuku ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza baada ya kutembelea banda la REA katika sherehe hizo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, ameipongeza REA kwa juhudi kubwa inazoendelea kuzifanya katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia nchini. Amesema miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira. Ameeleza kuwa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ni hatua muhimu katika kuboresha afya za wananchi, kulinda mazingira pamoja na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira kwa kiwango kikubwa. Aidha, ametoa rai kwa wananch...

SERIKALI YATANGAZA MIRADI YA LIGANGA NA MCHUCHUMA KUANZA RASMI MWAKA HUU WA FEDHA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali imekamilisha majadiliano ya utekelezaji wa Mradi Unganishi wa Chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma kupitia mwekezaji mpya wa Kampuni ya Shudao Investment Group Company Limited (SDIG) kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Amesema kupitia majadiliano hayo, pande zote zimefikia makubaliano muhimu kuhusu mgawanyo wa hisa, muundo wa uwekezaji, usimamizi wa mradi, kiwango cha mtaji pamoja na uongezaji thamani wa madini ya chuma, vanadium na titanium hapa nchini. Aidha, rasimu za mikataba ya ubia (JVAs) na wanahisa (SHAs) tayari zimekamilika huku hatua za mwisho za idhini zikiendelea katika mamlaka husika. Serikali inatarajia mikataba hiyo kusainiwa katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 kabla ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi utakaotekelezwa...

Serikali Yatangaza Miradi ya Liganga na Mchuchuma Kuanza Rasmi Mwaka Huu wa Fedha

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali imekamilisha majadiliano ya utekelezaji wa Mradi Unganishi wa Chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma kupitia mwekezaji mpya wa Kampuni ya Shudao Investment Group Company Limited (SDIG) kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Amesema kupitia majadiliano hayo, pande zote zimefikia makubaliano muhimu kuhusu mgawanyo wa hisa, muundo wa uwekezaji, usimamizi wa mradi, kiwango cha mtaji pamoja na uongezaji thamani wa madini ya chuma, vanadium na titanium hapa nchini. Aidha, rasimu za mikataba ya ubia (JVAs) na wanahisa (SHAs) tayari zimekamilika huku hatua za mwisho za idhini zikiendelea katika mamlaka husika. Serikali inatarajia mikataba hiyo kusainiwa katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 kabla ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi utakaotekelezwa...

Kapinga: Tunaleta Intelijensia ya Masoko

  WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema Serikali imepanga kuanzisha Kitengo cha Intelijensia ya Masoko na Viwanda kwa lengo la kuimarisha ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa. Akizungumza leo Mei 22, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri Kapinga amesema hatua hiyo inalenga kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za masoko, teknolojia na fursa za biashara duniani. “Katika mazingira ya sasa ya ushindani wa biashara na viwanda duniani, taarifa sahihi za masoko na teknolojia ni msingi muhimu wa maendeleo ya sekta ya viwanda na biashara,” amesema Kapinga. Amesema Serikali imebaini changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa taarifa za masoko ya kimataifa, mahitaji ya bidhaa katika misimu tofauti, viwango vya ubora pamoja na vikwazo vya kibiashara. “Kumekuwapo changamoto ya kutokujua bidhaa zinazohitajika katika misimu mbalimbali, viwango vya ubora na vikwazo vya kibiasha...