Skip to main content

Posts

Showing posts from July 23, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kairuki Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani

Na Mwandishi Wetu - Zambia Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism) Kanda ya Afrika, Bi. Elcia Grandcourt. Pamoja na mambo mengine  kikao hicho kilijikita katika kuendeleza ushirikiano na Shirika hilo hususan, fursa na programu mbalimbali za  chombo hicho katika maeneo ya uendelezaji wa mazao ya utalii, utangazaji utalii, kuvutia uwekezaji katika miundombinu ya utalii na huduma, utoaji wa mafunzo na kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya utalii. Kikao hicho kilimefanyika leo  katika Hoteli ya Avani Victoria Falls Resort, Jijini Livingstone Zambia na  kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kitaalam wa UN, Bw. Jaime Mayaki,  Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii,  Bw. Richie Wandwi pamoja na Afisa Utalii wa UN Tourism, Bi. Zineb Remmal.

Majaliwa: Serikali ina Mahusiano Mazuri Na Sekta Binafsi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema maendeleo yaliyopo nchini hivi sasa yametokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya Serikali na sekta binafsi. “Maendeleo tunayoyaona nchini kwetu katika kila sekta yanategemea mchango wa Serikali pamoja na sekta binafsi. Dhamira na maono ya Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuimarisha sekta binafsi ili ihuishwe na kuwa mshindani katika kuleta maendeleo makubwa kwa nchi yetu,” amesema. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumanne, Julai 23, 2024) wakati akizungumza na wadau wa sekta binafsi nchini kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sekta Binafsi Tanzania kwa mwaka 2024 yaliyofanyika Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.  Wiki ya Sekta Binafsi Tanzania inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 25 ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). Amezitaka wizara na taasisi za Serikali ziendelee kupokea maoni ya sekta binafsi na kuhakikisha yanazingatiwa katika marekebisho ya sera na sheria za biashara ili kuondoa vikwazo vya urasimu na...

Mhandisi Rogatus Mativila Azitaka Halmashauri Zote Nchini Kusafisha Barabara na Mitaro

Serikali imezitaka Halmashauri zote nchini kutambua kuwa jukumu la kusafisha  barabara na mitaro ni la kwao na si la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) huku wananchi wakihimizwa kuzitunza barabara zinazojengwa katika maeneo yao. Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI  anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa barabara na madaraja zilizojengwa kwenye kata ya Kibakwe wilayani Mpwapwa. Mhandisi Matavila amesema kwamba Halmashauri zielewe kwamba suala la kusafisha barabara zilizojengwa kwenye Halmashauri, Miji na Majiji yao ni jambo la kwao na hivyo wanatakiwa kuhamasishana  waweze kusafisha. “Tumeshaletewa barabara nzuri tuzitunze ili zitusaidie sisi wenyewe, mwananchi una nyumba hapo pembeni ya barabara ni vyema kujitoa kusafisha hizo nyasi kandokando ya barabara”, amesisitiza

George Marato Tv Yapata Mwaliko Kushuhudia Mapokezi ya Meli Vita Tatu Toka China

Kituo cha Cha habari za Mtandaoni Cha George Marato TV  leo Julai 24,2024 kimekuwa ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyopata mwaliko wa mapokezi ya Meli vita tatu za Jeshi la Uukombozi wa watu wa  China. George Marato Mkurugenzi Mtendaji wa George Marato Tv ni Miongoni Mwa wawakilishi wa Vyombo Vya habari hapa Nchini vilivyopata mwaliko Kushuhudia Mapokezi hayo Katika bandari ya Dar es Salaam. Ujio wa meli vita hizi tatu ni kutoka Jeshi la ukombozi la watu wa China inatokana na ushirikiano ulipo na jeshi la ulinzi wa wananchi Tazania JWTZ ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jwtz

Wanafunzi Toka Bunda na Serengeti Wanufaika na Mafunzo ya Uhifadhi Maliasili na Mazingira Toka Grumeti Fund

Na Emmanuel Chibasa Tafiti mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (HAKIARDHI) pamoja na wadau wa mazingira na mashirika mengine  kuanzia mwaka 2013 zinaonyesha viashiria vya kuthibitisha kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi kutokana na Vipindi vya mvua kubadilika mara kwa mara, Kukauka kwa vyanzo vya maji, Ongezeko la joto pamoja na Kutotabirika kwa majira ya mwaka nk. Mabadiliko ya tabia nchi ni mabadiliko ya hali ya hewa ya muda mrefu katika eneo fulani (Mkoa, Nchi au Bara) tofauti na iliyozoeleka na Mabadiliko hayo huleta athari katika nyanja za kiuchumi, kimazingira na kijamii, kutokana na mwenendo wa uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi yanatokana na uharibifu wa maliasili na mazingira. Wataalamu wa masuala ya mazingira wameainisha vyanzo vya kiasili na shughuli za kibinadamu ambavyo vinasababisha mabadiliko ya tabianchi kutokea. Miongoni mwa shughuli hizo za binadamu ni pamoja na uvunaji wa misitu usio endelevu kwa ajili ya biash...

Waziri Kairuki Aongoza Ujumbe wa Tanzania Kushiriki Mkutano wa Shirika la Utalii Duniani

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Pili wa Shirika la Utalii Duniani - Kanda ya Afrika (Brand Africa ) Kuhusu Utangazaji Utalii unaoongozwa na mada isemayo: "Kuitangaza Afrika kwa lengo la kufungua fursa za Uwekezaji na Maendeleo ya Sekta ya Utalii".  Pamoja na mambo mengine mkutano huo umejadili masuala ya kukuza utangazaji utalii na taswira ya Bara la Afika kwa kuandaa  maudhui yanayoliuza Bara hilo lengo ikiwa ni kuvutia watalii wengi zaidi. Mkutano huo unafanyika leo Julai 23, 2024 katika hoteli ya Avani Victoria Falls Resort, jijini Livingstone Zambia ukihusisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kutoka nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani. Mhe. Kairuki ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Ephraim Mafuru, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Richie Wandwi pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wiz...

Kocha Mkuu wa Biashara United Fc Ashiriki Kozi ya Ukocha Diploma A ya CAF

Kocha Mkuu wa timu ya Biashara United ya Mara Aman Josiah Leo ameanza Kushiriki Kozi ya ukocha ngazi ya Diploma A ya CAF  Kozi hiyo ambayo itafanyika Kwa kipindi Cha Mwaka Mmoja inafanyika Tanga na inaendeshwa chini ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF inahusisha makocha 25 kutoka nchi Mbalimbali za afrika na wakufunzi Zaidi ya Sita kutoka FIFA  Katika Picha Kutoka kushoto ni Kocha Msaidizi wa Timu ya Yanga Moussa N'Daw, Katikati ni Kocha Mkuu wa timu ya Azam Fc Youssouph Dabo na Kulia ni Kocha Mkuu wa Biashara United Aman Josiah wakiwa Katika Picha ya Pamoja huko Tanga 

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Wiki ya Sekta Binafsi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 23, 2024 ni mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Wiki Maadhimisho ya Wiki ya Sekta Binafsi inayofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.

TIC Yatoa Semina Kwa Wafanyabiashara Juu ya Fursa za Uwekezaji Mkoani Mara

Na Shomari Binda-Musoma KITUO cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) kimeendesha semina kwa wafanyabiashara mkoani Mara juu ya kuwa wawekezaji na kupata fursa zikiwemo unafuu wa kodi. Semina hiyo iliyofanyika leo julai 23 kwenye ukumbi wa uwekezaji, imefunguliwa na mkuu wa mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi na kusisitiza wafanyabiashara kuja kuwekeza mkoani Mara. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mtambi amesema mkoa wa Mara unazo fursa nyingi za uwekezaji nchi kavu na majini na ni sehemu salama ya kuwekeza. Amesema asilimia zaidi ya 70 ya hifadhi ya Serengeti ipo mkoani Mara hivyo kuna nafasi kubwa ya kufanya uwekezaji wa kitalii. Kanali Mtambi amesema licha ya eneo la nchi kavu lipo ziwa victoria ambapo unaweza kufanyika utalii wa majini na shughuli za uvuvi ukiwemo wa vizimba. " Tunawakaribisha sana kituo cha uwekezaji mkoani Mara kutoa semina kwa wafanyabiashara wetu ili nao wawe wawekezaji kwenye nchi yao.  Mkoa wa Mara zipo fursa nyingi za kufanya uwekezaji kikubwa ni wafanyabiash...

Bunge la India Kutoa Fursa Zaidi za Mafunzo Kwa Watumishi wa Umma

Bunge la India limeahidi kutoa fursa zaidi za mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa umma kupitia Taasisi yake ya Utafiti na Mafunzo ya Kidemokrasia (PRIDE) inayoendeshwa na Bunge hilo.  Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 23 Julai, 2024 na Spika wa Bunge la India (Lok Sabha), Mhe. Om Birla wakati wa mazungumzo yake na Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika Ofisi za Bunge hilo Jijini New Delhi. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe. Birla amemuelezea Dkt. Tulia kuhusu maboresho yaliyofanywa na Taasisi hiyo  ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya ufadhili kwa Watumishi wa umma kutoka nchini mbalimbali Duniani hususani Wabunge na Watumishi wa Mabunge ya nchi hizo.  Vilevile, Mhe. Birla ametoa kipaumbele mahususi kwa Watumishi wa Tanzania kwa kuzingatia urafiki, historia na uhusiano uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na India.  Aidha, kwa kutambua pia nafasi ya Dkt. Tulia kuwa Rais ...

Mtendaji Mkuu wa TARURA Victor Seif Awataka Watumishi Kufanya Kazi Kwa Bidii

Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa bidii  ili waweze kulinda taswira nzuri ya Wakala huo. Rai hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na watumishi wa TARURA mkoa wa Kigoma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa. Mhandisi Seff amesema kufanya kazi kwa bidii ni msingi wa kutekeleza majukumu ya Wakala na kuleta tija katika malengo na kukamilisha ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa ufanisi mkubwa. Aidha, Mtendaji Mkuu huyo amewapongeza wafanyakazi hao  kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwataka wasibweteke. Wakati huo huo Mhandisi Seff alitembelea  na kukagua barabara za Manispaa ya Kigoma  -Ujiji  na kumtaka Meneja wa TARURA Mkoa kuhakikisha wanazifanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara zilizojengwa ili kuzilinda na kuzifanya zidumu kwa muda mrefu.