Skip to main content

Posts

Showing posts from September 14, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

NDEJEMBI AONGOZA TANZANIA KWENYE JUKWAA KUU LA IAEA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiongoza kikao cha Maandalizi cha Viongozi na Wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania, wanaoshiriki Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA Scientific Forum) mara baada ya kuwasili Vienna nchini Austria leo tarehe 14 Septemba 2026. Makamu wa Rais, anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu ya Atomu (IAEA Scientific Forum) litakalofanyika tarehe 15 na 16 Septemba 2026 Vienna nchini Austria. Jukwaa hilo linafanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 70 wa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu ya Atomu (International Atomic Energy Agency - IAEA).

MFANYABIASHARA WA NISHATI YA GESI AIANGUKIA SERIKALI.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga  Mfanyabiashara wa nishati safi mkoani Tanga ameiomba serikali kuingilia Kati suala la uuzaji wa mitungi gesi ya kampuni tofauti tofauti katika eneo moja (kuchanganya mitungi) kwa wafanyabiashara wa rajareja. Rai hiyo imetolewa na Kamal Nandha mfanyabiashara wa kampuni ya Yogi Products Ltd aneyejihusisha na uuzaji na usambazaji wa nishati safi ya gesi kutoka kampuni ya Oryx gas. Nandha amesema ni vema Kila muuzaji akaamua kufanya kazi na kampuni Moja na sio kuchanganya kwani hii hupelekea aina nyingine kukosa wateja au kusuasua katika uuzaji wake pindi wanapochanganya. Nandha pia ameishukuru serikali Kwa hamasa wanayoitoa juu ya matumizi ya nishati safi ya gesi kwani imekuwa na matokeo chanya kwa wafanyabiashara wa nishati hiyo baada ya kuongeza mwamko kwa jamii. Pamoja na hayo pia ameiomba serikali kuangalia kwa jicho la tatu bei za gesi kwani bei zipo juu kulingana na hali halisi ya kipato cha mtanzania wa kawaida. "Ni vema serikali ingetoa ruzu...

WAZIRI MAKONDA ATEMBELEA BARCELONA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara maalum ya siku nne katika Klabu ya FC Barcelona nchini Hispania kwa mwaliko wa Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta. Makonda ameanza ziara hiyo tarehe 14 Septemba 2026 kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu kuhusu fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka nchini Tanzania. Mazungumzo hayo yalijikita katika maeneo ya kukuza vipaji, maendeleo ya kiufundi, uendeshaji wa timu ya taifa, pamoja na namna uzoefu wa Barcelona unavyoweza kusaidia maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Barcelona inatambulika duniani kwa mfumo wake wa kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji, jambo linaloifanya kuwa miongoni mwa klabu zinazotumika kama mfano katika maendeleo ya soka la kisasa. Aidha, sehemu kubwa ya wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania iliyotwaa Kombe la Dunia 2026 wametokea FC Barcelona. Katika ziara hiyo, Rais Laporta pia amempatia Makonda salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzan...

_DKT. MWIGULU: MFUMO MPYA WA UNUNUZI PAMBA UJULIKANE NDANI YA MWEZI MMOJA_*

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemuagiza Waziri wa Kilimo kukutana na wadau wa zao la pamba na ndani ya mwezi mmoja kuwasilisha mapendekezo ya mfumo bora wa ununuzi wa pamba utakaowanufaisha wakulima na kuendeleza uzalishaji wa zao hilo. Ametoa agizo hilo leo, Jumatatu Septemba 14, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Itilima, mkoani Simiyu, baada ya Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Daudi Silanga, kueleza changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba, ikiwemo malalamiko kuhusu mfumo wa sasa wa ununuzi. “Leo tarehe 14, mpaka tunapofika tarehe 14 mwezi ujao, niwe nimeshapata taarifa ya utaratibu mzuri ambao tutakubaliana,” amesema Dkt. Mwigulu. Amesema Serikali italinganisha mifumo iliyowahi kutumika na unaotumika sasa ili kupata utaratibu utakaokuwa na manufaa zaidi kwa wakulima bila kuathiri uzalishaji, bei ya pamba na maisha ya wananchi. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imeondoa sheria iliyokuwa ikiruhusu mifugo ya wananchi kutaifishwa na kuelekeza mapitio ya sh...

MKUU WA MKOA WA MARA BRIGEDIA JENERALI EVANS MTAMBI ATOA POLE KWA RAIS SAMIA

 Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans Mtambi hii leo amefika Kizimkazi Zanzibar kutoa salamu za pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha mumewe Ameir Hafidh Hassan kilichotokea hivi karibuni. Brigedia Jenerali Mtambi akiwa ameambatana na mkewe alipata fursa ya kutoa salamu za Wananchi wa Mkoa wa Mara pamoja na kufanya Dua ya pamoja na Viongozi wengine waliofika mahali hapo kwa lengo la kutoa salamu zao.

DC ITUNDA AMFARIJI NA KUMPA POLE RAIS DKT. SAMIA KUFUATIA MSIBA MZITO WA MUMEWE

 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, ameungana na majonzi ya Watanzania kwa kuwasilisha salamu za pole na rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba mzito wa kifo cha mume wake mpendwa. Katika kuonesha utu, heshima, na kuguswa kwa dhati na msiba huo, Mhe. Itunda amefika nyumbani kwa Mhe. Rais visiwani Zanzibar kwa ajili ya kumpa pole na kumfariji uso kwa uso katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwenza wake wa maisha.  Akiwa msibani hapo, Mhe. Itunda alimpa maneno ya faraja Mhe. Rais na familia yake, akimuombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira, afya njema, na nguvu ya kiroho ya kustahimili pigo hili kubwa.  "Tupo pamoja nawe katika kipindi hiki cha majonzi mazito, Mheshimiwa Rais. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akutie nguvu wewe na familia nzima, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahali pema peponi," yalielezwa sehemu ya maombi na salamu za faraja za Mhe. Itunda.