Skip to main content

Posts

Showing posts from July 31, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Maafisa Elimu Nchini Watakiwa Kuwa Waadilifu

Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amewataka Watendaji wa Mikoa, Halmashauri na ngazi ya msingi kuwa waadilifu, kujiamini na kufuatilia miradi ya maendeleo ili kuleta ufanisi na kulinda thamani ya fedha za Serikali.  Dkt. Msonde ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Julai, 2024 Chuo Cha Ualimu Patandi Jijini Arusha wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa Maafisa Elimu Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga, Maafisa TEHAMA na Waratibu wa Mradi ngazi ya Mkoa, Maafisa Elimu Sekondari, Maafisa Manunuzi na Ugavi ngazi ya Halmashauri, Waratibu wa mradi ngazi ya Halmashauri na Wakuu wa Shule kuhusu utekelezaji wa miradi ya shule za sekondari (SEQUIP).  “niwatake wasimamizi na wataalamu wote wa elimu na Idara mwambata katika usimamizi wa Miradi mkaimarishe usimamizi na kuongeza ubunifu katika utatuzi wa changamoto zinazoathiri shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule. Aidha, mkasimamie vema utekelezaji wa maboresho yanayofanyika mara kwa mara katika...

WAZIRI Mkuu Kufungua Maonesho ya Nanenane

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 01, 2024 anafungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni. Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Serikali Yaongeza Udahili wa Wanafunzi Taaluma za Afya Ngazi ya Kati

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeongeza udahili wa wanafunzi wa Taaluma za Afya ngazi ya kati, kutoka wanafunzi 20,030 mwaka 2020 hadi kufikia wanafunzi 25,390 ili kuounguza changamoto za upatikanaji wa watumishi wa kada hiyo.  Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Julai 31, 2024 wakati akitaja maazimio ya mkutano wa Siku Tatu wa rasilimali watu ulioandaliwa na Taasisi ya Hayati Benjamini Mkapa ikiwa ni kumbukizi ya alioyafanya katika Sekta ya Afya kwenye Ukimbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar aes Salaam.  "Wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo vikuu ngazi ya Shahada walikuwa elfu 5,674 mwaka 2023 ikilinganishwa na wanafunzi elfu 4,324 Mwaka 2020, hii itasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa watumishi inayopelekea wananchi kupata huduma kwa wakati." Amesema Waziri Ummy  Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imeongeza posho za madaktari anapoitwa nje ya saa za kazi, posho ya sare za wauguzi na ile ya kuchunguza mai...

Serikali Kusikiliza na Kufanyia Kazi Mahitaji ya Vijana Ili Kutatua Changamoto Zinazowakabili

Serikali imewaahidi vijana nchini kuwasikiliza na kuyafanyia kazi  mahitaji yao ikiwemo la ajira na mitaji ili kuwawezesha kundi hilo kufanya biashara na shughuli nyengine za kiuchumi na hivyo kuwezesha kuongeza kipato Chao. Ahadi hiyo kubwa imetolewa Jijini Dodoma na waziri ofisi ya waziri mkuu,anayeshughulikia, kazi,ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Ridhwani Kikwete kwenye kongamano la Vijana lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali inayoitwa #DOYODO ikishirikiana na wadau mbalimbali. Mhe. Kikwete ametumia Jukwaa hilo kuwaeleza vijana juu ya nia ya serikali kuendelea kuwahudumia vijana katika maeneo mbalimbali ya maisha yao na  utayari wake wa kukutana nao. Amesema uamuzi wa kukutana na vijana hao katika ngazi za chini za maamuzi zinalenga kukabili changamoto walizonazo kupitia programu mbalimbali zinazoendeshwa pamoja na marekebisho na sera na sheria ili ziendane na mahitaji yao ya sasa. Kongamano hilo kubwa limeshirikisha vijanan 632 kutoka mikoa yote nchini.

Serikali Yaahidi Kutatua Mgogoro wa Ardhi Kati ya Wananchi na Jeshi La Magereza Wilayani Ngara Mkoa wa Kagera

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepokea malalamiko ya mgogoro wa Ardhi kati ya Wananchi na Jeshi la Magereza katika Kijiji cha Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera. Kauli hiyo imetolewa Julai 30, 2024 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kutazama mgogoro uliopo baina ya Wananchi na Jeshi la Magereza. Mhe. Sillo amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nisikivu hivyo suala hilo la mgogoro huo atalifikisha katika vikao vya kamati ya maamuzi ili liweze kutatuliwa. “Niwaombe wakazi wa kata na Kijiji hiki cha Rusumo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapenda sana na sisi kama Wizara tumewekwa kwa ajili ya kumuwakilisha yeye ili kutatua changamoto zenu, suala hili la Mgogoro huu nimelichukua na tutalishughulikia”

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ampongeza Profesa Muhongo Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

  Na Shomari Binda-Musoma Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amempongeza mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Muhongo Kwa kutekeleza vizuri  Miradi ya Maendeleo Kwa Wananchi. Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava ametoa pongezi hizo wakati wa makabidhiano ya Mwenge, kwenye halmashauri ya wilaya ya Musoma kutoka manispaa ya Musoma leo julai 31 kwenye Kijiji cha Mmahare. Amesema wanatambua kazi nzuri inayofanywa na Profesa Muhongo katika kutekeleza majukumu yake kama mwakilishi wa wananchi. Kwenye eneo la mkesha wa mwenge kiongozi huyo amemzungumzia Profesa Muhongo kama mbunge anayefanya kazi na kuonekana ikiwemo kuziweka kwenye maandishi. Amesema salamu zake kama alivyozitoa atazifikisha kama zilivyo bila kupunguza chochote  kwa mheshimiwa Rais Dkt.Samia na kudai wamejifunza mazuri kwa mbunge huyo. Akizungumzia miradi 7 waliyoitembelea kukagua na kuweka mawe ya msingi ni miradi mizuri ambayo inakwenda kuwasaidia wananchi. Amesema wametembelea mradi wa za...

Rais Samia Amuapisha Kamishina Jenerali wa Magereza CP. Jeremiah Yoram Katungu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 31 Julai, 2024. Matukio Mbalimbali ya picha ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Kamishna wa Magereza CP. Jeremiah Yoram Katungu cheo Kipya cha Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 31 Julai, 2024.

Wakurugenzi wa Halmashauri Wapewa Mwezi Mmoja Kukamilisha Ujenzi wa Miundombinu ya Shule Mpya za Wasichana

Na. James K. Mwanamyoto Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa mwezi mmoja kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule mpya za sekondari za bweni za wasichana za mikoa ambazo zimejengwa katika halmashauri zao ili wanafunzi walioripoti katika shule hizo wapate mazingira bora na rafiki ya kupata elimu. Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akipokea taarifa za ujenzi wa shule hizo 26 za sekondari za wasichana za mikoa wakati wa kikao cha tathmini ya ujenzi wa shule hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Arnautoglo wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Mhe. Mchengerwa amesema, alitegemea wakurugenzi watoe taarifa ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hizo kwa asilimia 100 jambo ambalo halijatekelezeka, wakati yeye akiwa kwenye ziara ya Mhe. Rais Mkoani Rukwa alimuahidi Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ndani ya mwezi mmoja miundombinu ya shule zote 26 itakuwa imekamilika. Waziri Mchengerwa...