Na John Mapepele Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa rai kwa walimu nchini kuwa wazalendo na kuzingatia weledi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Mhe. Mchengerwa ametoa rai hiyo kwenye mkutano wa walimu na wadau wa elimu wa Wilaya ya Rufiji uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Bibi Titi Mohamed, ambapo yeye mwenyewe pia alitunukiwa tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake katika sekta ya elimu wilayani Rufiji. "Katika hali ya kawaida Serikali imeboresha mazingira na miundombinu ya sekta ya elimu kilichobaki ni kwa sisi walimu kutanguliza uzalendo ili kuinua kiwango cha elimu katika ngazi zote" . Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha, amesisitiza walimu kutambua wajibu wao na kwamba Serikali haitaweza kusita kuwachukulia hatua za kinidhamu Walimu na Maafisa Elimu ambao watakuwa wazembe katika utekelezaji wa majukumu yao. Katika taarifa ya Wilaya ya Rufiji kwa Mhe. Waziri, iliyoandaliwa na...
Marato tv - Sauti ya Jamii