Na Mwandishi wetu Jovina Massano Waganga wa tiba asili na mbadala hapa nchini washauriwa kusalimisha na kusajili nyara wanazotumia katika shughuli zao ili kuepuka adhabu na kukamatwa. Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Umoja wa Machifu Tanzania Mtemi Nyamilonda wa tatu Harun Mkomangwa jijini Mwanza mbele ya Mhifadhi mkuu Kituo Cha TAWA Mwanza kamanda Venance Mkamwa wakati wa zoezi la utoaji elimu ya uhifadhi iliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA). Mtemi Nyamilonda wa tatu amesema kumiliki nyara kihalali kutasaidia kuepuka adhabu za kukamatwa na faini kwa watumiaji zitakazopelekea kuwaondolea hofu katika uteketezaji wa majukumu yao. Aidha amewasisitiza viongozi walioshiriki katika zoezi hilo la elimu kuhakikisha wanawaelimisha waganga wa tiba asili na mbadala ambao hawakuweza kufika ili nao waweze kunufaika na umiliki nyara kihalali na kufuata miongozo taratibu na sheria zilizowekwa. "Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kutusikiliza ...
Marato tv - Sauti ya Jamii