Na, Mwandishi Wetu – Dar es Salaam Serikali inaendelea kuweka mkazo maalum kwenye kuboresha mfumo wa uratibu na upatikanaji wa mafunzo ya utarajali (internship) kwa kuwapatia wahitimu wa kada mbalimbali, uzoefu na ujuzi unaohitajika kwa lengo la kuwafanya wahitimu hao kuwa shindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi. Akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam Oktoba 22, 2026, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, amesema maboresho yanayoendelea kufanyika ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, aliyoyatoa wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma (C-COEs Forum 2026) tarehe 28 Septemba, 2026 jijini Arusha. Katika kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watenda...
Marato tv - Sauti ya Jamii