Na Mwandishi Wetu
DOHA, Qatar
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechaguliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) kuanzia 2027–2030, baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika tarehe 16 Novemba, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU - PP 26).
Ushindi huu unaashiria na kuthibitisha dhamira ya nchi katika kuendeleza mawasiliano ya simu duniani na maendeleo ya kidijitali. Nchi Wanachama 175 wa ITU walipiga kura katika mkutano huo, na kuchagua Baraza la Wajumbe 48 kwa miaka minne ijayo kuanzia 2027-2030. Viti kumi na vitatu kati ya hivyo vimetengwa kwa Kanda D, Afrika ambapo Tanzania ilipata nafasi ya kuwa mjumbe kwenye baraza hilo kwa kura 131.
Serikali inaendelea kutumia fursa hii kuchangia kwa ufanisi katika uongozi wa kimataifa wa TEHAMA huku ikikuza matarajio ya kidijitali ya Tanzania, Afrika na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki.





Comments
Post a Comment