NaMwanamkuu Mwandoro, Tanga.
WANANCHI mkoani Tanga na mikoa jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika uchunguzi wa awali na matibabu ya upasuaji kwa atakaebainika na changamoto ya Busha/Ngirimaji bila malipo kuanzia Novemba 16 hadi 30,2026.
Akizungumza na waandshi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi. Dkt. Batilda Burian amesema serikali imeandaa Kambi maalimu kwajili ya kuwafikia wananchi wengi wenye changamoto hiyo ili kuweza kupatiwa matibabu kwa urahisi,pia matibabu hayo yanatarajiwa kutolewa katika wilaya tatu za mkoa huu ambazo ni Handeni, Muheza na Korogwe.
Aidha Dkt. Batilda amesema ugonjwa wa ngirimaji husababishwa na vimelea vinavyoenezwa kwa binadamu kupitia kung'atwa na mbu waliobeba vimelea vya maambukizi, hali inayoweza kusababisha kuvimba kwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na kuziba kwa mfumo wa limfu.
Ameongeza kuwa madhara ya ugonjwa huo yanaweza kuathiri afya za waathirika, shughuli zao za kiuchumi, ustawi wa familia na maisha ya kijamii,
na kuwa tangu kuanza kwa kambi za upasuaji wa mabusha/ngirimaji mwaka 2009, jumla ya wagonjwa 14,454 wamepatiwa huduma nchini kote, wakiwamo 1,517 kutoka Mkoa wa Tanga.
Pia Dkt. Batilda amewataka wananchi kuendelea kuweka mazingira yanayo wazunguka katika hali ya usafi ili kuweza kupunguza mazalia ya mbu kwani itasadia kupunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo hilo kwa jamii.
Amemalizia kwa kusema kuwa utekelezaji wa kambi hizo utafanyika kwa ushirikiano wa Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) pamoja na wadau wengine wa afya.
Kwa upande wake mratibu wa ugonjwa wa matende na mabusha kutoka wizarani Dkt. Gulinja Antony amesema uwepo wa kambi hizo umekuwa ukisaidia sana kwani wagonjwa wengi ni watu wenye hali gumu za maisha hivyo wanapofikiwa kama hivyo na kupatiwa matibatu huwasaidia sana.
Amesema kambi hizo zinawapa wagonjwa fursa ya kufanyiwa uchunguzi na kupata huduma za upasuaji katika maeneo yao, bila kulazimika kutumia gharama kubwa kusafiri kwenda umbali mrefu kutafuta matibabu.
Ameendelea kuwasisitiza wananchi wenye changamoto hiyo kujitokeza katika hospitali zitakazotoa huduma hizo, huku akisisitiza umuhimu wa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya na kuepuka njia zisizo salama za matibabu.
Hospitali zitakazo toa huduma hizo ni hospitali ya Halmashauri ya Handeni vijijini itakayoanza tarehe 16 - 22, na kufuatiwa na wialaya Muheza baada ya handeni na kutamatisha huduma katika wilaya ya Korogwe na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kwa wananchi



Comments
Post a Comment