Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.
Katika kuhakikisha Dira ya maendeleo ya 2050 inafanikiwa na kila mwananchi kuishiriki vema kuna umuhimu mkubwa wa kuhamasisha Kilimomisitu.
Katika kongamano la Kitaifa la kumi na moja la Kilimo Misitu ambalo limelenga kuimarisha mazingira ya kisera yenye ustahimilivu kwa maendeleo ya kilimo nchini limeendelea kuwezesha fursa ya ajira kwa makundi mbalimbali hapa nchini.
Bidhaa nyingi zimeletwa na makundi mbalimbali yanayojihusisha na kilimo,ufugaji na usindikaji.
Mtandao wa Vikundi vya wakulima na wafugaji Nyancha( MVIWANYA) ni miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo ambao wameweza kuleta bidhaa mbalimbali.
Mratibu wa Shirika la MVIWANYA Joel Nguvava amesema makongamano kama haya yanawajengea uwezo wakulima na wafugaji pia na kubadilishana uzoefu kupitia mafunzo mbalimbali yanayopelekea kuboresha shughuli zao.
"Tunapata fursa ya masoko na wateja wapya na kutuwezesha kuongeza kipato na ajira kwa vijana",amesema Nguvava.
Kwa Upande wake Ester Renard mjasiriamali wa ungalishe kutokea wilaya ya Serengeti ambae ni mmojawapo wa MVIWANYA amesema kongamano limewezesha kujifunza zaidi na kupata ubunifu wa namna bora ya kuongeza thamani ya bidhaa zake.
Amewashauri Vijana kuwa na uthubutu wa kuona fursa mbalimbali hasa kilimo misitu kwa kuwa ni mkombozi wa ajira na kukuza uchumi na kujiletea Maendeleo.
France Gulaka Samwel ni miongoni mwa Vijana waliopo MVIWANYA ambae anajishughulisha na ufundi wa viatu vitokanavyo na ngozi za ng'ombe na za wanyama mbalimbali kutokea wilaya ya Rorya.
Amesema kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa malighafi za kutengeneza bidhaa za viatu kuna changamoto kwa kuwa hupata kutoka Dodoma na Morogoro Hali ambayo inapelekea ghalama kuongezeka ikiwemo usafiri.
" Ninaomba wizara husika hasa ya viwanda kupitia serikali ya awamu ya sita kuweka mpango mkakati wa kuweka kiwanda cha kuchakata ngozi kwa kuwa mkoa wetu wa Mara unazalisha ngozi kwa wingi kutokana na uwepo wa Ng'ombe,mbuzi na kondoo kwa kiasi kikubwa hii itasaidia unafuu wa ghalama,"amesema France.
Ameongeza kuwa wizara husika itenge maeneo kwa vijana ili uzalishaji uongezeke na kuongeza ajira kwa vijana wengi na kuwa sehemu ya kushiriki kwa vitendo dira ya maendeleo 2050.
Akimalizia Afisa Miradi wa MVIWANYA Joseph Bugwema ameishauri jamii kujitahidi kufika na kupata taarifa mbalimbali kwa kuwa kwa kiasi kikubwa jamii inategemea kilimo mbinu mbalimbali hutolewa zenye kumwezesha mwananchi kupata njia sahihi na suluhisho katika kilimo.
Hakusita kuipongeza serikali kwa kushirikiana na Vi Agroforestry kwa ushirikiano waliouonyesha kuanzia maandalizi hadi hitimisho la kongamano.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni" Kilimo misitu kwa vijana na Uwekezaji".
Kwa maelezo hayo imeonyesha namna gani kilimomisitu imewezesha uzalishaji wa bidhaa nyingi ikiwemo mbolea asili kutoka katika mabaki yatokanayo na vyakula mbalimbali.
Na hii ni fursa kwa vijana kuona namna bora ya kujiajiri na kuwa wawekezaji.








Comments
Post a Comment