UVCCM Mkoa wa Mara imemshukuru Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb.), kwa mchango wake katika kuunga mkono na kuchochea juhudi za maendeleo katika Mkoa wa Mara.
Shukrani hizo zimetolewa na UVCCM Mkoa wa Mara chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mhe. Mary Daniel Suráti (Mb.), ikieleza kuwa mchango wa Dkt. Nyansaho kupitia Nyansaho Foundation umekuwa sehemu ya juhudi za kuleta maendeleo katika mkoa huo.
UVCCM imesema mchango huo unaendelea kuwa chachu ya maendeleo na mfano wa uzalendo na kujitolea katika kulitumikia Taifa.
Aidha, UVCCM imemtakia Dkt. Nyansaho afya, hekima na nguvu zaidi katika kuendelea kulitumikia Taifa na kushiriki katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo


Comments
Post a Comment