Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga
Mfanyabiashara wa nishati safi mkoani Tanga ameiomba serikali kuingilia Kati suala la uuzaji wa mitungi gesi ya kampuni tofauti tofauti katika eneo moja (kuchanganya mitungi) kwa wafanyabiashara wa rajareja.
Rai hiyo imetolewa na Kamal Nandha mfanyabiashara wa kampuni ya Yogi Products Ltd aneyejihusisha na uuzaji na usambazaji wa nishati safi ya gesi kutoka kampuni ya Oryx gas.
Nandha amesema ni vema Kila muuzaji akaamua kufanya kazi na kampuni Moja na sio kuchanganya kwani hii hupelekea aina nyingine kukosa wateja au kusuasua katika uuzaji wake pindi wanapochanganya.
Nandha pia ameishukuru serikali Kwa hamasa wanayoitoa juu ya matumizi ya nishati safi ya gesi kwani imekuwa na matokeo chanya kwa wafanyabiashara wa nishati hiyo baada ya kuongeza mwamko kwa jamii.
Pamoja na hayo pia ameiomba serikali kuangalia kwa jicho la tatu bei za gesi kwani bei zipo juu kulingana na hali halisi ya kipato cha mtanzania wa kawaida.
"Ni vema serikali ingetoa ruzuku na upande wa gesi kama ilivyofanya katika bidhaa za kilimo na dawa ili kusaidia bei kuwa rafiki kwa watanzania wote kulingana na hali ya maisha ilivyo Kwa wananchi wake", alisema Nandha.
Kwa Upande wake mtumiaji wa nishati ya gesi Fatma Hussein kutoka maeneo ya chumbageni wilaya ya Tanga amesema wanapata wakati mgumu katika kufanya maamuzi wanafika dukani na kukuta mitungi aina zote dunkani.



Comments
Post a Comment