Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga.
Vijana wapatao 80 kutoka katika wilaya zote mkoani Tanga kunufaika na mradi wa ufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi kutoka katika chuo cha VETA Tanga,mradi uliopo chini ya taasisi ya Islamic Help Tanzania ambapo watapatiwa mafunzo katika fani nne ambazo ni ufundi umeme wa majumbani,umeme wa magari,ufundi Bomba pamoja ufundi garage.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwa ya muda wa miezi sita huku yakihusisha vijana wa kiume pekee lengo ikiwa ni kuwakwamua kiuchumi na kuwaepusha na mkundi hatarishi,mradi huo umefadhiliwa na Shirika la International Islamic Charity Organization 'IICO' lililopo nchini KUWAIT huku ufadhili huo utahisisha gharama zote za masomo.
Akizungumza na waandshi wa habari afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka shirika la Islamic Help Tanzania Salum Shaibu amesema kuwa lengo la ufadhili huo ni kuwasaidia vijana ambao licha ya kumaliza elimu ya Sekondari wameshindwa kujiendeleza kimasomo kutokana na hali ya familiya kushindwa kumudu gharama za kuwapeleka vyuoni jambo ambalo litasaidia kupunguza vijana tegemezi waliopo mtaani bila shughuli za kufanya ambazo zinaweza kuwapatia kipato.
"Lengo la Islamic Help tukishirikiana na IICO wafadhili wetu ni kuwasaidia wazazi kuondokana na mzigo wa ada ambao wangewalipia vijana wao na tunaamini kwamba mradi huu utawanufaisha vijana hawa kiuchumi na dhamira yetu baadaye tutatoa kozi nyingine kwa vijana wengi zaidi awamu inayofuata" amesema Shaibu.
Shaibu pia ameiomba Serikali kuwashika mkono pale ambapo watakwama katika kutekeleza miradi yao ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuisaidia jamii katika kukabiliana na hali duni ya kimaisha ikiwemo kuwasaidia vijana kupata elimu ambayo itakuwa ni chanzo cha kujitoa katika makundi hatarishi.
Sambamba na hayo pia Shaibu amewataka wazazi na walezi kuliunga mkono Shirika hilo juu ya vijana wao ambao wamepata ufadhili huo wa masomo kwa kuhakikisha kuwa licha ya kulipiwa ada wanawahimiza kushiriki masomo darasani kikamilifu na kuweza kufanya vizuri ili watakapo maliza waweza kupata ujuzi utakaowawezesha kujipatia kipato.
Kwa Upande wake Oscar Kaihura kijana kutoka katika wilaya ya Lushoto ambaye amepata nafasi ya ufadhili katika mafunzo ufundi wa umeme wa majumbani amesema analishukuru shirika la Islamic Help Tanzania kwani alikuwa na ndoto za kuja kuwa fundi mkubwa wa umeme na anaona ndoto zake zinakuja kutumia huku akiwataka vijana wenzake waliokosa nafasi hii kuwa na subra kwani nao pia watakuja pata katika awamu zijazo.




Comments
Post a Comment