Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid akiwa kwenye kikao kazi na Kansela wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Ndugu Xu Sujiang, leo Jumatatu tarehe 27 Aprili 2026, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupokea ugeni wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CPC na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Liu Haixing, anayetarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Tanzania, mwezi Mei 2026.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.








Comments
Post a Comment