S2kizzy Atangaza Albamu Mpya Inayokwenda kwa Jina la "Virus"
Producer na msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva, S2kizzy, ametangaza ujio wa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Virus
S2KIZZY Leo oktoba 9,2026, amesema mbele ya waandishi wa Habari kuwa anatarajia kutoa Album mpya inayotajwa kuwa na mabadiliko makubwa, mtindo mpya, na sauti ya kipekee itakayowashangaza na kuwafurahisha mashabiki.
Amesema Sifa Kuu za Albamu ya Virus
Mabadiliko na Ubunifu na vionjo kedekede ambavyo havijawai kutokea kwenye Tasinia ya mziki wa Bongo freva
Amesema albamu hii ina sauti ya tofauti na ni fenomena, ikileta mabadiliko, muonekano mpya (artwork/front view), na mwelekeo wa kipekee kwenye muziki.
Ameongeza kuwa Ushirikiano yaani (Collabs za Kipekee): Albamu hiyo inajumuisha ngoma kali za kolabo, ambapo kwa mara ya kwanza ngoma yake na msanii Nandy imepatikana kupitia albamu hii, mbali na kolabo nyingine nyingi zenye mshangao.
S2KIZZY amewataka mashabiki kujiandaa kwa vitu vingi vipya na vya kushtukiza ambavyo hawakuwahi kuvifikiria, ikiwemo kusikia wasanii mbalimbali kwenye mitindo mipya.
Msukumo kwa Producer wa Kitanzania: Mradi huu unatajwa kuwa ni mwamko, movement, na msukumo mkubwa kwa producers wa Kitanzania ili kuonesha uwezo mkubwa wa kutengeneza kazi kubwa zaidi kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijacho.
Amesema Tarehe rasmi ya kuachia albamu hiyo itatajwa hivi karibuni, huku S2kizzy akiwakaribisha wadau na mashabiki kuipokea kazi hii mpya.
Mwisho


Comments
Post a Comment