▪️Awasaidia kusajili SACCOS ya wakina mama
▪️Achangia Tsh 10m
▪️Wakina Mama wampongeza Rais Samia kwa mikopo nafuu
📍Mtumba, Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mhe.Anthony Mavunde ameendelea kuwa bega kwa bega na Wananchi wake kwa kutimiza ahadi zake alizowaahidi Wananchi hao katika kuwainua kiuchumi na kuwajengea uimara katika shughuli za kiuchumi.
Jana tarehe 1 Agosti 2026, Mbunge Anthony Mavunde amefanya kikao na wakina mama wa kata ya Kiwanja cha Ndege na kuwataka kuendeleza umoja na mshikamano ili kujenga SACCOS imara ambayo mwisho wa siku itasaidia kubadilisha maisha ya wakina mama hao.
Akiwa kama Mlezi wa SACCOS hiyo Waziri Mavunde ambaye ndiye Mbunge wao amewasaidia Tsh 10,000,000 ili kufanikisha usajili wa SACCOS hiyo na kuwasogezea fursa mbalimbali ikiwemo mikopo nafuu inayotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ha uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wananchi wote wa Tanzania, akiamini kwamba kupitia SACCOS hiyo wataweza kukopesheka na kunyakua fursa nyingi za kiuchumi hivyo kuchochea maendeleo yao na Kaya zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wabunge wa viti maalum Mh.Dkt. Neema Majule na Mhandisi Aisha Msantu wameahidi kuwaunga mkono wakina mama wa K/Ndege SACCOS kwa kufanikisha mafunzo ya uanzishwaji wa miradi na pia kuchangia Tsh 1,000,000 kwa kila mmoja.
Naye Mwenyekiti wa SACCOS ya Kiwanja Cha Ndege Bi. Priscila Baraka amempongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mipango mizuri ya kuwainua wakina mama kupitia mikopo ambayo inaratibiwa na serikali na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kukosa mitaji ya uhakika kuendesha shughuli zao.












Comments
Post a Comment