Pia, walizungumzia ushirikiano na kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya madini ambapo kwa upande wa Ghana asilimia 60 ya uzalishaji unafanywa na wachimbaji wadogo na asilimia 40 unafanywa na wachimbaji wakubwa, hali inayowanufaisha wananchi wa kawaida.
Kuhusu Biashara baina ya nchi mbili kuwa na muamko mdogo, waligusia kuendelea kuipa msukumo mkubwa na hasa baada ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kuanzisha safari katika ukanda huo wa Magharibi ambapo kumeanza kuchochea fursa mbalimbali za kiuchumi tofauti na awali.



Comments
Post a Comment