Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Mamlaka za kiserikali zimetakiwa kutoa elimu zaidi kwa jamii ili kuepusha uharibifu wa miundombinu ya serikali ikiwemo reli,mabomba ya maji na umeme.
Hayo yamesemwa na mkurungenzi wa kampuni ya Migungani company limited inayojishughulisha na ukusanyaji taka rejeleshi (chuma chakavu,oil chafu na chupa za maji) Bwana. Johannes Alexander Chacha iliyopo jijini Tanga.
Chacha ametoa kauli hiyo kufuatia changamoto wanazopitia kutokana na biashara wanayofanya ya chuma chakavu,wao ambao wanafata Sheria zote na kuwa na vibali pia hujikuta wanatiwa matatizoni.
"Niiombe serikali kusimamia vema sheria zilizowekwa katika biashara hii ya taka rejeleshi kwani itasaidia kuwatambua hata wale wanaofanya biashara hii kinyume cha Sheria",alisema Chacha
Aidha chacha pia ameishukuru serikali Kwa kuwaona na kuwapa kipaumbele pale inapokuja miradi ya kimkakati kama ujio wa Bomba la mafuta ghafi linaloendelea kujengwa huko chongoleani,kwani wao ni wadau wa kubwa wa maendeleo katika mkoa wa Tanga na wanachangia pato la taifa kwa kulipa kodi tangu kuanzishwa Kwa kampuni Yao ambayo mpaka sasa ina miaka isiyopungua mitano.
Nae afisa rasilimali watu wa Migungani company Janeth Mirumbe ameiomba serikali kuangalia Kwa hicho la tatu gharama za vifaa kinga kwani bei zake sio rafiki na kupelekea kama kampuni kutumia gharama kubwa kuwavalisha wafanyakazi wake.
Mirumbe pia ametilia mkazo Kwa serikali katika utambuzi wa mali za serikali ili kuepusha migongano inayoweza kujitokeza mara Kwa mara pia ameongeza kuwa kazi inayofanywa na kampuni Yao inasaidia Kwa kiasi kikubwa kuweka mazingira ya jiji la Tanga katika hali ya usafi.
"Pamoja na kwamba kazi hii inatuingizia kipato lakini pia inasaidia katika kupunguza kama sio kuindoa kabisa taka katika mazingira na kuyaacha yakiwa safi na salama kwani wananchi wameichangamkia sana fursa hii", alisema Mirumbe.
Kwa Upande wake mfanyakazi wa Migungani company limited Godlav Mollel ameishukuru ameishukuru kampuni hiyo kwani imekuwa mkombozi wa vijana wengi na yeye akiwa mmoja wapo kwani sasa anajipatia kipato ambacho kinamsaidia kutunza familia na kufanya mambo mengine.
Kampuni ya Migungani mpaka sasa imesaidia kupunguza wimbi la vijana mtaaani wasio na shughuli za kufanya na kufanikiwa kutoa ajira Kwa vijana 35.



Comments
Post a Comment