Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DC MSOFE ATOA ONYO KALI KYERWA: ‘TUKIUUA MNADA, TUNAUA BEI YA KAHAWA'


 Na Angela Sebastian,Kyerwa

MKUU wa Wilaya ya Kyerwa, Zaitun Msofe, amewataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuongeza nguvu katika kudhibiti magendo ya kahawa na mianya yote inayosababisha Halmashauri kukosa mapato, akisema vitendo hivyo vinadhoofisha uchumi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla.

Msofe alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kilichojadili utekelezaji wa shughuli za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Alisema Kyerwa ipo katika msimu wa biashara ya kahawa, zao ambalo ni tegemeo kubwa kwa wakazi wa Wilaya hiyo na chanzo muhimu cha mapato ya Halmashauri, hivyo madiwani wanapaswa kufuatilia kwa karibu biashara zinazoendelea katika kata zao na kuhakikisha wafanyabiashara wanatimiza wajibu wa kulipa ushuru.

“Tuko katika kipindi cha msimu wa biashara hii ambayo tunaitegemea sana Kyerwa katika kukusanya mapato,Kahawa ndiyo zao kubwa tunalolitegemea hapa kwetu hivyo madiwani nawakumbusha kuwa wapo baadhi ya watu wanaofanya biashara hii na kukwepa kulipa ushuru wa Serikali kwa kuvusha kahawa na kuuza kwa majirani zetu,” alisema Msofe.



Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alisema amepokea taarifa za baadhi ya wakulima kukusanya kahawa na badala ya kuipeleka katika Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS), wanakwenda kuiuza kwa watu binafsi wanaoweka mizani majumbani kinyume cha utaratibu.

“Ningependa tushirikiane kuhakikisha hatufanyi hujuma kwa hizi AMCOS zikakosa kahawa na matokeo yake zikafa. Pia tuangalie kwamba hatuendi kuua mnada,” alisema.

Msofe alisema baadhi ya AMCOS za maeneo ya mpakani zimeruhusiwa kununua kahawa kwa fedha taslimu kwa sababu maalumu, lakini akasisitiza kuwa utaratibu huo hautakiwi kutumiwa na wafanyabiashara wote kwa sababu unaweza kudhoofisha mfumo wa minada.

“Kabla ya mnada bei ilikuwa chini na kahawa haikuwa na thamani tukiruhusu kila mtu kununua kwa fedha taslimu, tunaua mnada na mnada ukifa, kinachofuata ni kuua bei ya kahawa kwa sababu kila mwenye pesa atanunua kwa bei anayoijisikia,” alisema.

Katika hatua nyingine, Msofe aliwataka madiwani kufuatilia kwa karibu miradi mbalimbali inayotekelezwa na jamii katika maeneo yao, akisema baadhi ya miradi imekuwa ikikabiliwa na changamoto katika utekelezaji.

Alisema fedha zinazotumika katika miradi hiyo ni fedha za umma, hivyo ni muhimu kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Bahati Henerico, alisema Halmashauri hiyo imefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Alisema Halmashauri imekusanya na kupokea Sh bilioni 51.1, sawa na asilimia 108 ya lengo la Sh bilioni 47.1, fedha ambazo zimetumika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali, ikiwemo miradi ya maendeleo hadi Juni 2026. 

Henerico alisema mapato ya ndani yamefikia Sh bilioni 7.9, sawa na asilimia 101, ikilinganishwa na lengo la Sh bilioni 7.7 ambapo mafanikio hayo yametokana na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Halmashauri katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha vyanzo vyote vinachangia ipasavyo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Jemsi John, alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayowanufaisha wananchi huku akiwashauri madiwani kuendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi wa Halmashauri ili kufikia malengo ya kuwapatia wananchi huduma bora na stahiki.

Kwa upande wao, baadhi ya wakulima na wananchi wa Kyerwa wameishauri Serikali kuweka mkakati wa kuhakikisha wakulima wanapowasilisha kahawa zao kwenye AMCOS wanalipwa kwa wakati, badala ya kuambiwa wasubiri malipo kwa muda mrefu wakati huo wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji fedha.

Rachel Mukama, mmoja wa wananchi, alisema elimu kwa wakulima na wananchi kuhusu madhara ya utoroshaji wa kahawa ni muhimu, sambamba na kuboresha bei ya zao hilo ili kuwafanya wakulima kuona faida ya kuuza kupitia mfumo rasmi.

Alisema uzoefu wa nchi jirani unaonyesha kuwa bei nzuri inaweza kuwa kichocheo muhimu cha kuwafanya wakulima kuuza kahawa kupitia njia halali na kuongeza mapato kwa Serikali na wananchi.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...