hatua hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu za Serikali kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimeti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema msaada huo utaiwezesha Tanzania kuongeza usalama wa taarifa za Serikali, kurahisisha upatikanaji wa nyaraka kwa wakati, kuhifadhi kwa ufanisi kumbukumbu muhimu za taifa kwa muda mrefu na kuboresha utoaji wa huduma za umma kupitia mifumo ya kidijitali.
"Vifaa hivi vinaimarisha mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali, vinaongeza usalama wa taarifa muhimu za taifa na kuboresha ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Amesema Kikwete
Aidha, mchango huu unaonyesha kuendelea kuimarika kwa uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Tanzania na Sultanate ya Oman," amesema.
Mhe. Kikwete amesema Mbali na manufaa ya kiteknolojia, makabidhiano hayo yanalenga kuwa ni kielelezo cha ushirikiano unaozidi kuimarika kati ya mataifa hayo mawili katika maeneo ya maendeleo ya taasisi za umma, utunzaji wa kumbukumbu na matumizi ya teknolojia ya kisasa.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali ya Tanzania na Oman, akiwemo Balozi wa Sultanate ya Oman nchini Tanzania, Mheshimiwa Said Hilal Al-Shidhani, Balozi Abdallah Kilima kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na viongozi na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka.




Comments
Post a Comment