RC MALIMA: MAANDALIZI YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI YAFIKIA ASILIMIA 99, AWATAKA WAKULIMA KUZALISHA MAZAO KWA KUZINGATIA MAHITAJI YA SOKO
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, leo Julai 30, 2026 ameongoza kikao cha tatu cha Kamati Kuu ya Maandalizi ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kanda ya Mashariki 2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa JKT Nanenane, Manispaa ya Morogoro.
Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Mhe. Malima alizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua za maandalizi ya maonesho hayo yanayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 1, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mhe. Malima aliwahimiza wakulima kuzalisha mazao yanayokidhi mahitaji ya soko la ndani na la kimataifa ili kuongeza tija, ushindani na mchango wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi.
Aidha, amesema maandalizi ya maonesho hayo yamefikia asilimia 99, huku maboresho makubwa ya miundombinu na mazingira ya maonesho yakikamilishwa kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wakubwa kuonesha bidhaa zao katika mazingira bora na kuwapa fursa ya kutambulika zaidi pamoja na kupanua masoko ya bidhaa zao.
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, biashara na teknolojia, Kwa lengo la kuhamasisha ubunifu, kuongeza uzalishaji na kuchochea maendeleo ya uchumi kupitia sekta ya kilimo.





Comments
Post a Comment