Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga
Waziri wa nishati Mh. Deogratius Ndejembi amemtaka mkandarasi aneyetekeleza ujenzi wa njia ya umeme utakao tumika katika uendeshaji wa mitambo kuhakikisha anakamilisha kazi hiyomwanzoni mwa mwezi wa nane.
Agizo hilo amelitoa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Africa mashariki (EACOP) katika eneo la chongoleani ambapo mpaka sasa mradi umefikia 87% ya ujenzi.
Waziri Ndejembi pia amewataka wananchi kuchangamkia fursa zitokanazo na mradi huo,huku ikionekana kwa kiasi kikubwa mradi umeitoa ajira hasa Kwa watanzania, watanzania wakionekana kuwa asilimia 84 na huku asilimia 30 ikiwa ni wakazi wa chongoleani.
"Watanzania niwaombe kuulinda mradi huu kwani ni mradi mkubwa sana kiuchumi na umechangia katika ukuzaji uchumi Kwa jiji la Tanga kwani umeweza kutoa ajira na kuwapatia ujuzivijana wa kitanzania,ujazi ambao wanaweza kutumia katika ujenzi wa miradi migine kama hii", Ndejembi.
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amesema miradi mikubwa kama hii husaidia katika kuimarisha huduma za jamii kwani Kwa kupitia Bomba la mafuta wameweza kujenga kituo cha afya na timu ya coastal union wameweza kujipatia uwanja wa mpira.
Pamoja na hilo amempongeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan Kwa usimamizi madhubuti wa mradi huu ambao unaelekea ukingoni katika kukamilika kwake ambapo mwezi wa nane mwaka huu unatakiwa kuwa umekamilika.
Mradi huo wa Bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda mpaka choleani mkoani Tanga unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka huu na huku ikitarajiwa meli ya kwanza kuchukua mafuta ghafi kutoka chongoleani mwezi January 2027.





Comments
Post a Comment