Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga
WANANCHI mkoani tanga wametakiwa kuthamini fedha zinazowekezwa na serikali katika ujenzi wa miundombinu hasa barabara.
Wito huo umetolewa na meneja wa TARURA mkoa wa Tanga George Tarimo alipokuwa akitoa taarifa ya miradi ya barabara inayotarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru na mingine kuwekewa jiwe la msingi.
"Gharama zinatotumika ni kubwa sana sasa ni vema wananchi Kila mmoja akawa milinzi wa mwingine,kutotupa taka katika mitaro ambayo husababisha mitaro hiyo kuziba na kuharibika Kwa Barbara kitu ambacho ni hasara Kwa serikali",alisema Tarimo.
Aidha Tarimo alisema kuna miradi nane ambayo itapitiwa na mwenge wa uhuru mwaka huu ambayo ipo katika wilaya ya Kilindi,Pangani Handeni ,Korogwe, Lushoto,Bumbuli Muheza na Tanga jiji.
Pamoja na hayo pia mradi wa Kilindi Dc ni Daraja ambalo lipo kwenye (hatua ya Box), na barabara ya mapanga Mlingotini ambayo gharama yake ni milioni 22.5 ambayo inajengwa na mkandasi Negron Buiders Company limited .
" Mradi wa barabara ya Chanika Kilole DSD yenye KLM 1.7 Handeni Tc ambayo inajengwa katika kiwango cha lami inagharimu kiasi cha sh. bilioni 1.17 ambapo mwenge utaweka jiwe la msingi , mradi ambao unajengwa na wakandarasi wawili Jp Traders limited alitumia kiasi sh.milioni 720 na Atimo Costractioni Limited alikitumia kiasi cha sh.milioni 451." alisema Tarimo
Aliongeza kusema kuwa miradi mingine ni pamoja na mradai wa ujenzi wa kiwango cha lami DSD barabara ya Mnyongeni Wilayani Pangani yenye urefu wa kilometa 0.75 na kugharimu sh.milioni 475 huku ikijengwa na Mkandarasi Atimo Contraction Co.LIMITED na ujenzi wa kiwango cha lami DSD ya barabara ya Kange 2 yenye urefu wa Km.2.4 yenye huku ikigharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.36 ikijengwa na Mkandarasi The Globalink General Contraction limited.
Hata hivyo Tarimo alisema kuwa Mradi wa ujenzi wa Daraja hadi sasa umefikia hatua ya ( Box Culvert ) barabara ya Bombani- Kiwanda ambayo inagharama ya sh.milioni 47 inajengwa na mkandarasi Mwallow Company limited ambapo ujenzi wa mradi wa kiwango cha lami DSD ya barabara ya Halmashauri ya Korogwe TC yenye km 0.65 inagharimu milioni 475 yenyewe inajengwa na Mkandarasi RISO BUSINESS HOLDING CO.LIMITED.
Tarimo alisema Miradi mingine ni ya ujenzi wa daraja la Usambara katika barabara ya Vulini Kirilicha -Kwindoghoi yenye gharama ya milioni 449 ambayo kazi yake imekamilika chini ya mkandasi KIV Company limited,huku mradi wa ujenzi wa kiwango cha lami DSD barabara ya Shambala-Dochi imegharimu kiasi cha shilingi milioni 993.9 ambayo inajengwa na Mkandarasi Gloda Contraction Costractioni Limited.
TARURA imesema kuwa miradi yote hiyo imegharimu takribani kiasi cha shilingi bilioni tano.

Comments
Post a Comment