Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Operesheni Jeshini, Kanali Victor Magare pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Jeshini, Kanali Herry Juma Masokola, ambao wamefika mkoani Mara kufanya tathmini ya hali ya kiusalama na kuangalia namna vikosi vilivyo tayari kulinda mipaka ya nchi.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mhe. Mtambi aliwakaribisha wageni hao na kuwahakikishia kuwa Mkoa wa Mara uko salama, huku wananchi wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu.
Ameongeza kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana kwa karibu na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa, hususan katika maeneo ya mipakani.
Ujumbe huo wa MMUT unaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa.




Comments
Post a Comment