Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 18 Juni 2026, jijini Mombasa, Kenya, wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa 11 wa Masuala ya Bahari (Our Ocean Conference), ambapo alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema mkutano huo umeimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto za bahari, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza uwekezaji, teknolojia na ujenzi wa uwezo wa taasisi ili kutumia kikamilifu fursa za Uchumi wa Buluu kwa maendeleo endelevu.
Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Serikali ya Kenya kwa kufanikisha mkutano huo na kusisitiza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kulinda bahari na kuendeleza Uchumi wa Buluu jumuishi na endelevu.
Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alijumuika Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Samoei Ruto, katika dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa katika hoteli hiyo kwa viongozi na wageni walioshiriki mkutano huo.






Comments
Post a Comment