Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Mwenge wa Uhuru unatarajia kuwasili mkoani Tanga June 17 mwaka huu katika kijiji cha Mtoro Kata ya Tunguri wilaya ya Kilindi ukitokea mkoani Morogoro.
Ukiwa mkoani hapa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri 11 kwa umbali wa kilometa 1340 ukikagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya misingi katika miradi 73 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 27
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian amesema baada ya kukamilisha mbio zake mkoani hapa Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa mkoani mkoani Kilimanjaro June 28 mwaka huu.
"Mwenge huu wa Uhuru utaweka mawe ya misingi jumla ya miradi 34, utafungua na kuzindua jumla ya miradi 26, utatembelea na kukagua jumla ya miradi 11 ya shughuli za vijana na miradi miwili ya maendeleo ya sekta ya maji, miradi hii yote ina jumla ya thamani ya shilingi bilioni 27, milioni 764, laki 390 na 480.01" Amesema Batilda.
"Ujumbe wa mwenge kwa mwaka huu wa 2026 unahusu ujenzi wa amani, umoja na mshikamano wa kitaifa chini ya kauli mbiu isemayo "Tanzania ni yetu sote tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo"

Comments
Post a Comment