Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga
Jamii mkoani Tanga imetakiwa kutojiingiza katika mahusiano yatakayo kuja kuvunja haki za wengine.
Hayo yamesemwa na mratibu chama Cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) mkoa wa Tanga ambae pia ni mwanasheria Mwanaidi Kombo kutokana na ongezeko kubwa na wanaume wanaotelekeza familia hasa watoto.
Huku akisema kwasasa hiyo imekuwa changamoto kubwa na wamekuwa wakipokea kesi nyingi kuhusu wanaume kutohudumia watoto.
Mwanaidi aliongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya watoto,Sheria namba 21 ya mwaka 2009 katika kifungu Cha 9(1),kimeeleza wajibu wa mtoto kuishi na wazazi wake lakini pia wajibu wa wazazi kumhudumia mtoto yale mahitaji muhimu ya kibinaadamu kiwemo,chakula,malazi,mavazi na elimu pamoja na huduma za matibabu.
Pia katika 9(2)wameelekeza kuwa mzazi ama mlezi atakae kuwa na mtoto katika malezi atawajibika kumpatia mtoto hayo mahitaji,na katika kifungu Cha 33-41 kimeelekeza wajibu wa mzazi ama mlezi,afisa maendeleo ya jamii,kuhakikisha mtoto anapatiwa ulinzi na huduma stahiki.
Pia amewatahadharisha wanaume kuhusu kuona kama wanaonewa katika jukumu la kumhudumia watoto,kwani mama hutumia muda wake mwingi katika kumhudumia mtoto ambapo baba huyo angetakiwa kumlipa mtu wa mkulelea mtoto wake ingekuwa ni gharamazaidi na huwenda asingeweza kabisa.
"Kwa Tanga sasa hivi imekuwa kawaida Kwa wanaume kutotoa huduma Kwa watoto,hii zaidi ni Kwa wale ambao hawaishi pamoja kwani wanakuwa na Imani ya kuwa anapotoa mahitaji ya mtoto basi atamuhudumia na mama mtoto kitu ambacho sio kweli Kwa hali ya maisha ilivyo sasa na hela anayotakiwa kutoa huwa haiwezi kukidhi hata hayo mahitaji ya mtoto wake", Mwanaidi
Amemalizia Kwa kuwataka wanaume kuwa wawazi katika mahusiano kwani sio kila mahusiano yanahitiji mtoto mengi yapo kwaajili ya kukidhi mahitaji ya kimwili na ni haki ya Kila moja kujua na kutumia uzazi wa mpango,hii itasaidia kupunguza migogoro inayoepukika katika mahusiano.
"Wanawake wengi kinachowapa fahari wanapoingia kwenye mahusiano wanaamini ni kubeba ujauzito wakati huo akili ya mwanaume hailengi huko,Kwa hiyo ni vema watu wakawa wazi kama ni kukaa na kupanga masuala ya maendeleo kwanza na watoto baadae ili kuepuka kuleta watoto watakao kuja kuteseka",. Mwanaidi


Comments
Post a Comment