Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Safari ya gridi ya Taifa ya maji imeanza, Wananchi tutunze vyanzo vya maji Kwa maendeleo


NA: DK. REUBENI LUMBAGALA

Ni dhamira ya kweli ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kumtua mama ndoo kichwani yaani kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika makazi yao na kuepukana na kadhia ya kuchota maji umbali mrefu.

Kwa lugha rahisi ni kwamba, Dk. Samia anataka wananchi wote wapate maji kwa asilimia mia moja. Kwa kuzingatia umuhimu wa maji, katika maisha na maendeleo ya binadamu, ni muhimu kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wote.

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji ambavyo mikakati madhubuti ikiwekwa, vinaweza kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi. 

Rais Dk. Samia akiwa mdau muhimu wa sekta ya maji, huku akichukizwa na namna wananchi wakiwemo wanawake na watoto wakitembea umbali mrefu kutafuta maji, ameipa Wizara ya Maji jukumu la kuhakikisha inatekeleza mradi wa Gridi ya Taifa ya Maji.

Rais Dk. Samia ametolea mfano Wizara ya Nishati ilivyo na Gridi ya Taifa ya Umeme, ndivyo Wizara ya Maji inapaswa kuwa na Gridi ya Taifa ya Maji. 


GRIDI YA TAIFA YA MAJI NI NINI?

Ni mfumo wa kitaifa unaounganisha miundombinu ya maji kutoka vyanzo vikubwa vya maji vya uhakika kama maziwa na mito ili kusambaza maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali kwa maendeleo.

Kupitia mradi huo, maji yatatolewa Ziwa Viktoria kuelekea mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara na Arusha. 

Kutoka Ziwa Nyasa, maji yatapelekwa mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Njombe, Iringa, na Mbeya.

Vilevile, maji yatatoka Ziwa Tanganyika kuelekea mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa na Songwe.

Kama hiyo haitoshi, Mto Rufiji nao utasaidia kupeleka maji mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga na Morogoro.

Hii yote ni kuhakikisha maji yanatolewa kutoka vyanzo vikubwa vya maji kama mito na maziwa na kuwafikia wananchi wote vikiwemo vijiji 1,575 vilivyosalia ifikapo mwaka 2030.


VIONGOZI NA WATENDAJI WA MAJI WAFANYA ZIARA CHINA KUJIFUNZA GRIDI YA TAIFA YA MAJI 

Mwezi Machi, 2026, timu kutoka Wizara ya Maji wakiongozwa na Waziri wake, Jumaa Aweso, Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri na watendaji wengine, walifanya ziara ya mafunzo nchini China katika Jimbo la Shan Dong kujifunza namna ambavyo vyanzo vikubwa vya maji na maziwa vimeunganishwa katika Gridi ya Taifa ya Maji kutoka Kaskazini kwenda Kusini mwa China.

Mafunzo hayo ni muhimu wakati huu ambao  wataalamu wanahitaji uelewa kufanikisha usambazaji wa maji kutoka Ziwa Viktoria, Nyasa na Tanganyika. Pia, kutoka mito mikubwa ya Kagera, Rufiji, Ruvu, Wami, Ruvuma, Pangani na Kiwira ili yawafikie wananchi walipo kwa maendeleo. 


MFUMO WA UTABIRI WA KIASI CHA MAJI KWENYE MITO WAZINDULIWA

Machi 22, 2026, ikiwa ni Siku ya Kilele cha Wiki ya Maji nchini na Siku ya Maji Duniani, Makamu wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, alizindua Mfumo wa Utabiri wa Kiasi cha Maji kwenye Mito, Morogoro Mjini.

Aidha, mfumo huu utawezesha kupata taarifa sahihi za kiwango cha maji tulichonacho nchini ili kufanikisha mahitaji ya maji katika shughuli mbalimbali za maendeleo hasa kuelekea Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, ambapo Tanzania inakadiriwa itakuwa na watu milioni 118.


WABUNGE WAJENGEWA UWEZO MRADI GRIDI YA TAIFA YA MAJI



Hivi karibuni, wabunge katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma, walipewa semina kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Gridi ya Taifa ya Maji ikizingatia kuwa mradi huo unagusa majimbo na wananchi wao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri aliwaeleza wabunge mradi huo mkubwa namna utakavyowanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla. 

Aidha, wabunge walipewa taarifa kuhusiana na kukamilika kwa vipande vya mtandao wa taifa wa maji ambapo tayari maji yameanza kutolewa Ziwa Viktoria kuelekea Shinyanga, Tabora na maeneo ya Shelui mkoani Singida.


WANANCHI NA WAJIBU WA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

Wananchi tunao wajibu wa kulinda vyanzo vya maji ili kuhakikisha tunapata maji safi, salama na yenye kutosheleza kwa mahitaji ya maendeleo. Kimsingi, vyanzo vya maji vinapaswa kulindwa. 

Iko hivi: Walinzi wa kwanza wa vyanzo hivi ni sisi wananchi. Wananchi ndiyo wanufaika wa kwanza wa maji, kwahiyo, namna zozote za uhujumu na uharibifu wa vyanzo vya maji, ni kujidhulumu sisi wenyewe na kuchelewesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo zinarudisha nyuma kasi ya maendeleo.

Sambamba na hilo, wananchi tunao wajibu wa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kuhusu upotevu wa maji pale tunapoona maji yanamwagika na wizi wa maji unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

Kwa pamoja, tunaweza kufanikisha mipango mingi ya maendeleo katika sekta za kilimo, uvuvi, viwanda, miundombinu kama tutatunza vyanzo vya maji kwa maendeleo hasa kuelekea Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050 ambapo sekta ya maji ina sehemu kubwa kufanikisha mipango hiyo mizuri ya maendeleo.

Maoni: 0620 800 462.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...