Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Katibu wa Mbunge huyo, Mussa Hussein, amesema msaada huo umetolewa kwa lengo la kutatua changamoto ya upungufu wa Qur’an na vitabu vya dini katika misikiti ya Bunda Mjini.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za mbunge huyo za kuimarisha nyumba za ibada na kusaidia waumini kupata nyenzo muhimu za kujifunzia dini.
“Mheshimiwa Esther Bulaya amekuwa akitoa misaada mbalimbali katika misikiti ya jimbo letu na ataendelea kufanya hivyo. Mbali na msaada huu wa vitabu, pia kuna mipango mingine ya kuendelea kuboresha na kuimarisha nyumba za ibada pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili,” Amesema
Kwa upande wake, Sheikh wa kata ya Bunda stoo na Masjid Nuru Seif Haruna Musa Omar Kayege amepokea msaada huo kwa niaba ya waumini na kueleza kuwa Qur’an na vitabu hivyo vitakuwa mchango mkubwa katika kuendeleza mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Amesema msaada huo utaongeza upatikanaji wa vitabu vya kujifunzia na kufundishia dini, jambo litakalowasaidia waumini wengi kuelewa kwa kina mafundisho ya Qur’an Tukufu.
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Esther Bulaya kwa msaada huu. Mwenyezi Mungu amlipe kheri kwa kuunga mkono juhudi za kueneza elimu ya dini na kuwasaidia waumini wetu,” amesema Sheikh Kayenge.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake Nahmad iddi Mwanafunzi wa Madrasa Nuru Migungani wamemshukuru Mbunge huyo kwa kujitoa kwake ambapo wamesema kuwa vitabu hivyo vitakuwa msaada mkubwa katika kujifunza na kuelewa mafundisho ya dini ya Kiislamu, huku wakimuombea mbunge huyo aendelee kupata mafanikio katika kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo.
Wanafunzi hao wa Madrasa wakatumia nafasi hiyo kumuombea Kwa Mwenyezi Mungu Mbunge Esther Bulaya Kwa Msaada huo ambapo wamesema kuwa "Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma amzidishie Mbunge Esther Kwa mapenzi yake ya dhati na Mwenyezi Mungu amzidishie pale alipopunguza". Wamesema
Msaada huo ni sehemu ya mchango wa Mbunge Esther Bulaya katika kusaidia maendeleo ya kijamii na kuimarisha shughuli za nyumba za ibada ndani ya Jimbo la Bunda Mjini.





Comments
Post a Comment