Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mfumo utabiri kiasi cha maji nyenzo ya takwimu sahihi za maji


Na: Dk. Reubeni Lumbagala

Maji ni raslimali ya asili ambayo inatumika katika maeneo mengi muhimu yanayochagiza maendeleo. Upo umuhimu wa wananchi kuelimishwa ili kuielewa sekta ya maji kwa mapana badala ya kuona maji kama huduma ya kijamii pekee kwa shughuli za nyumbani kama kupikia, kufulia na kuogea.

 Maji ni zaidi ya matumizi hayo yaliyozoeleka kwa baadhi ya watu. Kwa nchi yetu yenye vyanzo vingi vya maji lakini wakati huo huo ina idadi kubwa ya watu na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi zinazohitaji maji, takwimu sahihi za maji zinapaswa kuwepo ili tusiwe watu wa kubahatisha kuelewa kiasi cha maji tulichonacho nchini na mahitaji halisi ya maji kufanikisha mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo. Bila takwimu sahihi tutakwama na hatutakuwa na uhakika wa kufanikisha mambo yetu kama nchi.

Katika masuala ambayo Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesisitiza kuyasimamia kikamilifu na kuyapa kipaumbele ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika shughuli mbalimbali za maji ili kuongeza kasi ya utendajikazi na ufanisi. 

Wizara ya Maji imekuja na teknolojia ya kisasa ya mfumo wa utabiri wa kiasi cha maji ya mito. Mfumo huu ulizinduliwa Machi 22, 2026, na Makamu wa Rais Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, katika Bwawa la Mindu Morogoro Mjini ikiwa ni kilele cha Wiki ya Maji Tanzania na Siku ya Maji Duniani. Mfumo huo ni teknolojia ya aina yake iliyokuja wakati sahihi.



Teknolojia hii ni muhimu hasa kipindi hiki ambacho mahitaji ya maji yameongezeka lakini pia kipindi hiki cha utekelezaji wa mradi wa Gridi ya Taifa ya Maji ikiwa ni agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunakuwa na Gridi ya Taifa ya Maji ambayo itapokea maji kutoka vyanzo mbalimbali vya maji na kuyatumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa maendeleo endelevu. Mfumo wa utabiri wa kiasi cha maji ya mito unatoa taarifa ya kiwango cha maji tulichonacho kama nchi. 

Hii itatupa picha kama kiasi kilichopo kinakidhi mahitaji ya Taifa au la. Na kama hakikidhi mahitaji, basi kama Taifa tutachukua hatua stahiki kuhakikisha tunaongeza kiwango cha maji ili kuepusha kukwamisha shughuli za kimaendeleo zinazohitaji maji kwa kisingizio cha upungufu wa maji. 

Ni muhimu kupunguza visingizio katika jitihada za maendeleo. Makamu wa Rais Dk. Nchimbi akisisitiza suala la usambazaji wa maji kwa wananchi kwani wanawake ni wahanga wakubwa. " Wanawake wana mchango wa kipekee shida ama Raha katika maji ni zaidi ya asilimia 60 wamekuwa watu wa maji usiku na mchana katika changamoto ya Maji na kutunza familia," amesema.


Kimsingi, mfumo wa utabiri wa kiasi cha maji ya mito nchini ni dira yetu kamili ya kuweka mikakati ya kujitosheleza kwa mahitaji ya maji. Kupitia mfumo huu, tutapata takwimu za kiwango cha maji kilichopo na kuongeza hamasa ya utunzaji wa mazingira pamoja na vyanzo vya maji ili tuendelee kuvuna maji zaidi kwa maendeleo ya sekta mbalimbali kama kilimo, viwanda, uvuvi, miundombinu, madini na shughuli nyingine muhimu za kijamii. Mikakati mizuri ya maendeleo iliyopo inategemea sana uwepo wa raslimalimaji.

Mathalani, shughuli za ujenzi kama barabara na madaraja zinahitaji maji. Kilimo cha uhakika kinategemea sana maji kwa ajili ya umwagiliaji. Uvuvi na mifugo inahitaji maji. Viwanda vinahitaji maji. Shule na hospitali zinahitajika maji. Uzalishaji umeme pia unahitaji maji. 

Maji yanagusa sekta nyingi za maendeleo. Kwa maneno mengine, kufanikiwa kwa mipango mizuri ya maendeleo kunategemea sana uwepo wa maji ya uhakika. Tunawezaje kuwa na uhakika wa kutumia maji katika shughuli za maendeleo kama hatuna taarifa za uhakika? Ndiyo maana mfumo wa utabiri wa kiasi cha maji ya mito umezinduliwa ili kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi za maji.

Kufanikiwa kwa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050 kunategemea sana upatikanaji wa maji safi, salama na yenye kutosheleza. Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, Dk. Nchimbi, inakadiriwa Tanzania kufikisha watu millioni 118 ifikapo mwaka 2050. Serikali itawezaje kuwahudumia wananchi wote hao na kutekeleza shughuli za maendeleo zinazohitaji maji pasipo kuwa na taarifa sahihi za hali ya upatikanaji wa maji nchini? Mfumo wa utabiri wa kiasi cha maji umekuja kujibu suala hilo. Pamoja na yote mazuri kuhusu sekta ya maji, suala la utunzaji na ulinzi wa vyanzo vya maji ni muhimu sana. 

Uhakika wa ulinzi na usalama wa vyanzo vya maji unachagiza kufikiwa kwa mipango ya maendeleo inayohitaji uwepo wa maji. Ni vyema wananchi tukawa mabalozi wazuri wa kutunza vyanzo vya maji na kutoa taarifu tunapoona upotevu wa maji katika maeneo mbalimbali ili hatua muhimu zichukuliwe kutatua changamoto hiyo. Sote tunategemea maji katika shughuli zetu za kila siku, tutakuwa wageni wa nani kama tutaharibu vyanzo vya maji? Ujio wa mfumo wa utabiri wa kiasi cha maji iwe ni hamasa ya kuongeza uzalishaji wa maji ili tuwe na maji ya ziara yenye kutosheleza mahitaji yote ya nchi na kuwa na ya ziada kwa maendeleo ya uhakika.

Maoni: 0620 800462.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...