DODOMA.
katika kutekeleza Maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,Serikali imetoa kibali cha ajira Kwa nafasi 12,000 za ajira zikiwemo nafasi 5,000 za kada za Afya na nafasi 7,000 za Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia ndani ya siku 100 za Serikali ya Awamu ya Sita.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo January 30,2026 Jijini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwan Kikwete, amesema kuwa kibali hicho cha ajira kilitolewa baada ya Rais Samia kuapishwa tarehe 3 Novemba 2025.
Amesema hadi sasa jumla ya watumishi 8,416 wameripoti katika halmashauri mbalimbali nchini, wakiwemo watumishi 3,694 wa kada ya elimu na watumishi 4,722 wa kada ya afya.
Sambamba na Hayo, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia tena kibali cha Ajira ya Watumishi 41,500 za watumishi wa Kada mbalimbali kama vile watumishi wa Kada za Afya, Walimu, Kilimo, Afya, Uvuvi, Wahandisi, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Polisi na watumishi wa kada mbalimbali.
"Naendelea kutoa rai kwa Watanzania wenye sifa kuendelea kujitokeza kwa wingi kuomba ajira katika Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma watapotangaza nafasi mbalimbali za ajira". Amesisitiza
Serikali itaendelea kutoa nafasi ya ajira na kuzitangaza ambapo imewataka vijana wote wenye sifa waendelee kuomba nafasi mbalimbali kwa kadri zitakapotangazwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Comments
Post a Comment