Mjumbe wa baraza kuu la UWT mkoa wa Mara Sister Yohana amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha Mapinduzi CCM kumteua awe mgombea udiwani viti maalum Manisoaa ya Musoma.
Sister Yohana ambaye ameshika nafasi mbalimbali za uongozi UWT kwa sasa mbali na kuwa mjumbe wa baraza UWT mkoa wa Mara pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Musoma mjini akitokea kata ya Mwisenge.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo,Sister Yohana amesema sasa ni wakati wake wa kutoa mchango kwa wanawake na makundi mengine ndani ya jamii kwa nafasi hiyo endapo chama chake kitamteua na kushinda nafasi hiyo.
"Mimi ni mjasilimali,najua changamoto nyingi zinazowakabili wanawake,Rais wetu na mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya Maendeleo pia kutoa fedhs za mikopo lakini bado kuna changamoto ya uhamasishaji wanawake kutumia fursa hiyo sasa ni wakati sahihi ya mimi kuwa diwani wa kundi hili niweze kusaidia wanawake wenzangu"alisema na kuongeza
"Najua nina vita kubwa lakini namwamini Mungu na chama changu,endapo nitateuliwa na kushinda nami nitoe mchango wangu kwa jamii katika kumsaidia Rais wetu mpendwa'"alisema.







Comments
Post a Comment