Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM kutokea wilaya ya Rorya Sango Gungu Kasera leo Juni 30 mwaka 2025,amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kiweze kumteua kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Rorya mkoani Mara.
Sangu ambaye amefuta taratibu zote za uchukuaji wa fomu bila mbwembwe amefika katika Ofisi za ccm wilaya ya Rorya eneo la Utegi na kukabidhiwa fomu hizo na katibu wa ccm wikayani humo.
Hata hivyo baada ya taarifa kusikika za uchukuaji wa fomu kwa kada huyo wananchi eneo la Utegi walionesha shangwe kubwa huku wakiimba nyimbo za kabila la wajaruo za kumtakia kheri kada huyo katika safari hiyo ya kisiasa.
Tayari makada kadhaa wa ccm wamechukua fomu hizo za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Rorya akiwemo mbunge anayemaliza muda wake Jafari Chege.




Comments
Post a Comment