Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Awataka Maafisa Maendeleo Jamii Wasikubali Kuachwa Nyuma


📌 Awataka wafurukute  kuonesha umuhimu wa kadsa yao kwa Taifa

📌 Asema Wizara ya Nishati itashirikiana maafisa hao kusambaza umeme na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia 

📌 Rais Samia apongezwa kwa kuongeza ajira za maafisa maendeleo ya jamii

 

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza maafisa maendeo ya jamii nchini kushirikiana na kuhakikisha wanashirikishwa katika mipango ya nchi kuanzia ngazi za halmashauri na kuwezesha jamii kujiletea maendeleo endelevu na jumuishi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Mei 7, 2025 jijini Dodoma wakati aliposhiriki kwenye Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania.

“Mahali popote ulipo ni muhimu kila mtu ajue upo usisubiri uambiwe upo, ama litokee tatizo ndio waseme nani anaweza, wapeni ulazima wakuu wenu kuwatafuta  kupitia chama chenu furukuteni kwenye halmashauri zenu na mahali mlipo,” amesema Dkt. Biteko.

Amewaeleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuipa heshima taaluma yao kwa kuunda Wizara maalum ya kushughulikia maendeleo ya jamii.  Sambamba na kuongeza idadi ya ajira kwa maafisa hao zaidi ya asilimia 50 katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

Ametoa wito kwa Wizara, Serikali za Mitaa, Taasisi, Wakala, Mashirika na Tume nchini kutambua umuhimu wa kada hiyo kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya jamii “ Washirikiane kwenye kupanga maendeleo, wasiachwe nje bali wao ni wakala wa maendeleo,”

 Amesema licha ya  Maafisa hao kuwa wasajili wa wafanyabiashara wadogo, wasikubali tu kuwa wasajili wa NGO’s, au wasimamizi wa mikopo na kuitwa  wakati wa matatizo watu wanaposhindwa kurejesha mikopo badala yake wahakikishe wanashirikishwa pia katika mipango ya maendeleo.

Aidha, Dkt. Biteko amesema katika kuhakikisha kwamba maendeleo yanakuwepo katika ngazi zote za jamii kwa kutumia rasilimali zilizopo na katika kukabiliana na changamoto  Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuongeza ajira kwa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii ambapo kwa mwaka mwaka 2022/23 na 2024/2025 Serikali imeajiri jumla ya wataalamu 1500  ili kuboresha utendaji na utoaji huduma bora ngazi ya msingi.

Ametaja baadhi ya jitihada hizo kuwa ni kuanzishwa kwa Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na Kusimamia Maendeleo Ngazi ya Msingi wa Mwaka 2022/23 - 2025/26, Mpango unaolenga kuwafanya wananchi kuwa kitovu cha maendeleo ngazi ya jamii na Taifa.  Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) na Fursa mbalimbali za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Mazingira Wezeshi kwa Wadau kuchangia maendeleo.

Jitihada zingine za Serikali ni Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2024 – 2034, Mkakati unaolenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetoa ruzuku kwenye mitungi ya gesi ambapo wananchi wananunua mitungi ya gesi kwa nusu ya bei ya kuuzia katika maeneo ya wilayani na vijiji – miji ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha, Dkt.Biteko amesema kuwa Wizara yake itaendelea kushirikiana na maafisa maendeleo ya jamii nchini katika mipango yake ya kusambaza umeme sambamba na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Pamoja na hayo amewataka maafisa hao kuendelea na jukumu lao la kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi, kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuchangamkia fursa hizo muhimu ikiwemo Fursa ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), Mikopo ya Asilimia 10 ya Mapato ya Halmashauri kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu na  Mikopo ya wafanyabiashara ndogondogo.

“ Ninatambua kuwa moja ya jukumu lenu ni kwamba ninyi ni Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote nchini. Hivyo ninyi ni kiungo muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Mashirika hayo. Nataka nieleze mashirika hayo kuzingatia sheria na taratibu na wachukulieni hatua watakao kiuka,” amesema Dkt. Biteko.

Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Doroth Gwajima amesema kuwa Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ya jamii kutoka sekta ya umma na binafsi wapatao 1,238.

Amesema mafanikio yanayopatikana nchini ni sehemu ya  jitihada za maafisa maendeleo ya jamii kwa sababu maafisa hao wametangulia mbele katika kila sekta mfano elimu, ufugaji, afya, mila na utamaduni pamoja na uchumi kwa kubadili fikra na kuhamasisha wananchi ili waweze kushirikiana na Serikali katika mikakati ya maendeleo.

Ametaja lengo la Mkutano huo wa mwaka ni kubadilishana uzoefi na kupeana mbinu za kutekeleza majukumu yao.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatma Tawfiq amewapongeza maafisa maendeleo ya jamii kwa kufanya kazi kubwa  kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla, aidha Kamati yake itaendelea kuishauri Serikali kutoa fedha za kutosha ili maafisa hao wafanye kazi yao kikamilifu.

Pia, Mhe. Tawifiq amempongeza Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kuifanya Wizara ya Mendeleo ya Jamii kujitegemea na ameiomba Serikali kuwapa vitendea kazi maafisa hao mfano magari au pikipiki pamoja na kuiongezea bajeti Wizara hiyo ili maafisa hao waweze kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake, Rais wa Chama Cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA), Victor Kabuje amemshukuru Rais Samia kwa kufanya kazi kubwa ya kuwaletea Watanzania maendeleo

Amesema wataalamu wa maendeleo ya jamii wameendelea kuwahimiza na kuhamasisha wananchi wanashiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

“ Sisi kama  wataalamu wabobezi wa maendeleo ya jamii tunaendelea kuwa kubadilisha watu fikra na kuhamasisha maendeleo kuanzia ngazi ya familia na jamii, pamoja na kuhimiza wataalamu kuhamasisha wananchi katika matumizi ya nishati safi ya kupikia na tumegawa majiko kwa wananchi katika kila wilaya mfano kwangu nimegawa majiko 280,” amesema Kabuje.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...