Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Yakabidhi Hati Mbili za Mashamba ya Umwagiliaji


Serikali mkoani Mara imekabidhi hati mbili za shamba la umwagiliaji la Bugwema lililopo katika halmashauri ya Musoma vijijini kwa Tume ya Taifa ya  Umwagilaiji. 

Mashamba hayo ni maalumu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya shamba hilo ili liweze kutumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Shamba hilo ni  miongoni mwa mashamba matano ya mfano yanayotarajiwa kuanzishwa na Tume hiyo hapa  nchini kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.

Akikabidhi hati hizo leo Jumatano Mei 7,2025, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya ameiomba Tume hiyo kuhakiksha shamba hilo linaanza  uzalishaji haraka ili kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo na mkoa kwa ujumla.

Alisema Shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 3,000 limekaa kwa muda mrefu bila kufanyakazi. 

"Tayari tumekamilisha suala la umiliki wake tunaomba Tume ihakikishe uzalishaji unaanza mapema ili kuwanufaisha wananchi wa maenoe yale na watanzania kwa ujumla," amesisitiza. 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa akizungumza mara baada ya kupokea hati hizo amesema ujenzi wa miundombinu ya shamba hilo unatarajiwa kuanza kujengwa ndani ya wiki mbili zijazo.

Kwa mujibu wa Mndolwa, Serikali inalenga kulifanya shamba hilo pamoja na mengine manne kuwa ya mfano ili kuboresha kilimo cha umwaguliaji hapa nchini kutokana na umuhimu wake katika kukuza na kufanya sekta ya kilimo  kuwa endelevu. 

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya shamba hilo kutakuwa na utaratibu maalum wa kulima ambapo wakazi wa maeneo hayo watapewa kipaumbele sambamba na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

"Tukikamilisha ujenzi wa miundombinu tutakuwa na makundi mawili ya wakulima pale kwa maana wananchi wa kawaida wenye uwezo wa kulima heka moja hadi tano pamoja na wawekezaji wa kulima heka tano na kuendelea, kutakuwa na mfumo maalum na rafiki ambao utawezesha lengo hili la serikali kufanikiwa," amesisitiza 

Mndolwa amefafanua kwamba, shamba hilo la Bugwema lilianzishwa mwaka 1974 na Rais wa awamu ya kwanza hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ambapo liliwekewa miundombinu kadhaa yakiwemo mabomba lakini lilishindwa kuanza uzalishaji kutokana na sababu mbalimbali. 

"Serikali ya awamu ya sita imeona kuna umuhimu wa kufufua  shamba hili ili kuenzi maono ya Mwalimu lakini pia ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya kuboresha kipato cha mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla," amesema 

Ametaja mashamba mengine yanayotarajiwa kuwa mashamba ya mfano kuwa ni pamoja na shmaba la Chinamgali lililopo Dodoma, Kibondo  lililopo mkoani Kigoma,Mbarali na Madibila  mkoani Mbeya.

Amesema mashamba hayo yatawekewa miundombinu ya kisasa ili kuwezesha kilimo cha kisasa ambacho kitafanyika kwa mwaka mzima na kwamba baada ya mashamba hayo Tume hiyo inatarajia kuendelea kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji katika maeneo mengine nchini ili kuwanufaisha wananchi wengi zaidi.

Baadhi ya wakazi wa Musoma wameipongeza seeikali kwa hatua hiyo iliyofikiwa huku wakitaka  ujenzi wa miundombinu hiyo kukamilika kwa haraka na hatimaye shamba liweze kuanza uzalishaji. 

Mgosi Warioba amesema shamba hilo limekuwepo zaidi ya miaka 50 bila kuwanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa hivyo uamuzi wa kulifanya shamba hilo kuwa la mfano ni wa kupongezwa.

"Eneo ni zuri sana lipo  karibu na ziwa Victoria na mto Bugwema kwahiyo uhakika wa maji ni asilimia 100 wananchi tulikuwa tunasikitika eneo kukaa hivyo hivyo bila uzalishaji,niombe tu huu mchakato ukamilike haraka ili wengi waweze kunufaika," amesema 

Musa Amos amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi huo wakazi wa maeneo hayo wanastahili kupewa kipaumbele hatua ambayo mbali na kuimarisha uchumi wao pia itawasidia waweze kulima kisasa na kufaya kilimo chenye tija.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...