Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wanawake Chunya Wachangamkia Uchimbaji, Watoa Uzoefu, Ombi Kwa Serikali, Taasisi Za Fedha


*📍Chunya*

Sekta ya Madini nchini Tanzania inaendelea kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii na sasa inajulikana kama Sekta jumuishi inayotoa nafasi sawa kwa wote, wanaume, wanawake na vijana kushiriki kikamilifu. Wanawake Wilayani Chunya ni ushahidi wa mabadiliko haya, wakivunja dhana ya zamani kuwa madini ni kazi ya wanaume pekee.

Wakizungumza na Madini Diary hivi karibuni, baadhi ya wanawake hao wameeleza jinsi wanavyoshiriki katika kila hatua ya mnyororo wa madini: wapo wanaomiliki leseni za uchimbaji mdogo, wachimbaji mahiri, wapondaji wa mawe na wafanyabiashara. Wanasema shughuli hizo zimewawezesha kupata kipato, kulea familia, kuanzisha miradi ya maendeleo na kujenga makazi bora.Ushuhuda wao unaonesha wazi kuwa sekta ya madini inayoendeshwa kwa usawa wa kijinsia inaweza kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wachimbaji Wanawake  Itumbi-Chunya Happiness Mabula anasema “Mimi kwenda chini umbali wa mita 200 kuchimba madini ni kitu cha kawaida sana kwangu na nimefanya kazi hii si chini ya miaka 10, nina migodi yangu  na nimekua nikilipa kodi kwa Serikali kwa miaka yote na tunawasaidia vijana. Anaongeza kwamba, kama wanawake wananufaika na shughuli za madini na hivyo kuisaidia jamii. Licha ya mafanikio hayo anasema changamoto zipo kama kuvamiwa maeneo yao.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa kikundi hicho Angela Sompo anasema, ‘’kikundi chetu kilianza mwaka 2023 tukiwa wanawake 25, tulianza kwa kuwezeshana kwa kuchangiana vifaa kazi kama makarasha, compressor na mpaka sasa tumekwisha kutoa vifaa kwa wanachama 11 na vifaa hivi vimeturahisishia kazi zetu,’’ na anaongeza, ‘’tulianza kwa kuchangishana michango ya shilingi milioni 1 kila mwezi fedha zilizotusaidia kupata mitaji na kununua vifaa. Mbali na hayo,   Angela anasema amekuwepo kwenye shughuli hizo kwa miaka 10 sasa, anachimba kwenye leseni za mume wake ambazo umempatia mafanikio ya kiuchumi. Angela anasifu juhudi za Serikali kusimamia bei ya dhahabu na sasa wananufaika zaidi.

Kwa upande wa Kikundi cha Wachimbaji wanawake kijiji cha Itumbi iliyopo kata ya Matundasi-Chunya chenye makundi matatu ndani yake  ya Wema , Mafanikio na Malkia, Makamu Mwenyekiti wa kikundi Anna Francis anaishukuru Serikali kwa kuwapatia mashine ya kusaga mawe ambayo wameifanya kama chanzo cha mapato kwani inakisaidia kikundi cha kusaga mawe ya kototo kwa ajili ya shughuli za ujenzi. ‘’Tunauza kokoto gari moja la tani 10 kwa shilingi 300,000/ pesa hizo zinaingia kwenye mfuko wetu,". Mbali na vifaa, anaishukuru Serikali kupitia Chama Cha Wanawake Tanzania (TAWOMA) kwa kuwapatia nafasi ya kushiriki katika mikutano na makongamano hivyo kupata fursa ya kujifunza zaidi.

Ushiriki wake kwenye shughuli za madini umemuwezesha kusomesha watoto, kujenga nyumba na kuishi vizuri anasema  Mariam Hussein mmoja wa wanachama wa kikundi hicho na kuongeza," kuongezeka kwa bei ya dhahabu kumetusaidia sana, kwa gram moja sasa tunapata shilingi hadi Laki mbili na sitini  na kusema sasa uchimbaji umebadilika na Chunya imebadilika,".

Vikundi hivyo  vitatu tayari vimekwishapatiwa leseni moja ya uchimbaji mdogo iliyopo eneo la itumbi-Chunya bado ingawa bado hawajaanza kuchimba.


*Wanaume wanazungumziaje ushiriki wa Wanawake?*

 Samwel Jeremiah Mhasibu wa Chama Cha Wachimbaji Wadogo Wilaya ya Chunya  anasema‘’ Tunamshukuru Rais Samia kwa kuwainua wanawake, lakini Serikali kwa kuanzisha masoko ya madini ya dhahabu kwasababu yanawainua wachimbaji wakiwemo wanawake,". Anaiomba Serikali iwasadie wanawake kupata vifaa vya kuchimba.


*Mabadiliko Chanya kutokana na shughuli za Madini*

"Kutokana na ushiriki wa wa kina mama kwenye shughuli za madini, wameyaona mabadiliko ya wazi Chunya."Sekta ya madini imebadilisha sana Chunya. Chunya sasa ina majengo mazuri, kuna wawekezaji  wa kila aina, wa nyumba za biashara, makazi, kampuni za ulinzi, usambazaji wa vifaa. Chunya hii haikuwa hivi kabla,’’ anasema Sofia Mwanauta mwanamke mchimbaji wa madini Chunya na mmoja wa wanakikundi cha Wanawake wachimbaji Chunya .


*Ombi kwa Serikali na taasisi za fedha*

 Serikali itoe upendeleo kwa wanawake  kwa kuwapatia leseni za kuchimba zenye madini zilizofanyiwa tafiti ili wachimbe pasipo kubahatisha; wapatiwe elimu kuhusu mfumo wa kuomba leseni na malipo yanayotolewa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwawezesha kwa vifaa vya uchimbaji ili wasitumie nguvu kubwa kwenye shughuli za uchimbaji  na kwa taasisi za fedha wameiomba Serikali iendelee kuzungumza na taasisi hizo ili ziweze kulegeza masharti ya kukopa kwa Sekta ya Madini .  


*Pongezi kwa Serikali*

Vikundi hivi  vimeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasaidia kuweza kufanya kazi zao za uchimbaji kwa uhuru, amani na utulivu. Pia, Serikali kwa kusimamia bei ya dhahabu na kutokuwaacha nyuma wanawake. Aidha, wametoa shukrani kwa Serikali kuwapatia karasha pamoja na kuishukuru kwa kuwahamasisha kujiunga katika vikundi. Vilevile, wamepongeza  kwa kuanzishwa masoko ya madini na uwepo wa bei elekezi kwa kuwa yamerahisisha biashara ya madini.  Pia, wanawake Chunya wameipongeza Ofisi Madini Chunya kwa kuwasilikiza  wachimbaji na kutoa  ushirikiano mzuri bila ubaguzi.

*Wito kwa Wanawake Wengine*

Kutokana na manufaa wanayoyapata, wamewaasa wanawake wengine nchini kutokuogopa kushiriki katika  shughuli za madini. Wametoa hamasa kwa wanawake  kujiunga kwenye vikundi  ili kufikiwa na huduma kwa ajili urahisi licha ya kuwepo  mtazamo hasi kwa baadhi ya watu juu ya ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya madini, wanawake wachimbaji wanatoa hamasa kwa wengine ya kutokuogopa kwani wanaweza.



*#Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri*

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...