Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Alhamisi Oktoba 2,2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Mtwara kwa ajili ya kuanza ziara ya mikutano yake ya hadhara ya kampeni, kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani mkoani Mtwara baada ya kuhitimisha mkoa wa Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.











Comments
Post a Comment