Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Democratic Party (Dp) Yaahidi Kusamia Rasilimali Na Kufuta Kikokotoo


>Ameahidi kusimamia rasilimali za nchi

>Kuheshimisha utu na thamani ya mwanamke.

>Kuboresha Mishahara kuongeza ufanisi wa uwajibikaji.

>Kurudisha ujamaa

>Kufuata ndoto na nyayo za Rais wa awamu ya tano.


Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma

Mgombea  wa Urais kupitia Chama Cha Democratic (DP) Abdul Juma Mluya amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atasimamia rasilimali zilizopo kunufaisha wazawa na kuondoa kikokotoo kwa watumishi wa serikali.

Ameyasema hayo Septemba 30 akiwa ziarani mkoani Mara wakati akinadi sera zake na kuwaomba wananchi wa mkoa huu kumchagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema huduma zinazotolewa  hazikidhi haja za wananchi wa Tanzania kutokana na uwajibikaji mbovu wa viongozi kwa kuhujumu fedha za Umma.

Amesema endapo wananchi watamchagua hakutakuwa na tozo za janjajanja ataboresha huduma za Afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kutosha katika vituo vya afya nchini kote, huduma bora kwa akina mama wanakwenda kujifungua,wazee, watoto na watu wenye mahitaji maalum kwa kuondoa ghalama za matibabu.

Amesisitiza kuwa sio bure kwa sera na sheria halafu haitekelezeki itakuwa bure ili kuheshimisha utu , serikali ya DP itawajibika kutoa huduma ya lishe kwa mama atakaejifungua kwa muda wa miezi mitatu aweze kupata nguvu ya kumlea mtoto wake.

Ameahidi kuboresha mishahara kwa watumishi wa Umma wakiwemo walimu wauguzi na majeshi yote lengo ni kuongeza ufanisi na weledi kwa watumishi ili huduma za zipatikane kwa usawa.

Mishahara ikiboreshwa kwa watumishi wa Umma watakuwa na morali ya kuwatumikia wananchi kwa kuwa Mazingira ya kazi ni rafiki na kufanya kazi kwa starehe na yatapelekea kuondoa malalamiko kwa wananchi.

Upande wa elimu DP itaondoa michango kwa wanafunzi  na kutengeneza mazingira mazuri kwa walimu ili waweze kufundisha kwa ufasaha.

"Siku hizi wanafunzi wanaacha shule shuleni wanarudi na makaratasi nyumbani hii ni kutokana na mazingira duni kwa walimu hapa nchini", amesema Abdul

Kutokana na uwepo wa rasilimali za kutosha hapa nchini lakini wananchi wake wanaishi maisha duni kwa kuwa rasilimali zimegeuka adhabu na laana kwa wananchi wake DP itahakikisha  urithi wa watanzania utakuwa mikononi mwa wazawa wenyewe.

"Urithi wa rasilimali ulioachwa na waasisi wa Taifa ni lazima uwanufaishe watanzania mwekezaji anapokuja anapohitaji kuwekeza kipaumbele ni mchimbaji mzawa".

Uwepo wa madini ya aina mbalimbali hapa nchini kumekuwepo na wachimbaji wengi ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao na kujiongezea kipato na kujiletea Maendeleo.

Serikali ya DP itaweka utaratibu maalum utakaowezesha wachimbaji wadogo wadogo madini kuwa na haki ya kunufaika na madini wanayoyachimba kwa kupewa kipaumbele kwanza ndipo afuate mwekezaji,ubia umnufaishe mzawa kwanza.

Ameahidi kuondoa viwanja vya ndege vyote vilivyopo kwenye migodi kwa kuwa ni mojawapo ya viashiria vya wizi wa madini katika nchi.

"Watanzania tumeumbwa kuwa watu wa amani kwa nini tupoteze maisha kwa mali yetu ambayo Mungu ametupa ndio maana akayaweka madini nchini hayakuwekwa Ulaya".

DP itatengeneza Mazingira ya baadae kwa kuweka miundombinu ya ajira kwa Vijana kwa kufufua viwanda kwa kuwa rasilimali ni nyingi na malighafi zinapatikana hapa nchini,serikali madhubuti ni lazima ijenge uchumi imara kwa wananchi wake kwa kutumia rasilimali zilizopo kuleta Maendeleo.

Nchi hii imebarikiwa ardhi nzuri yenye rasilimali nyingi ambazo zikitumiwa kwa utaratibu mzuri  zitawezesha upatikanaji wa huduma bora na kujenga uchumi imara kwa nchi na wananchi.

Ametolea mfano nchi ya Cuba  inayotegemea zao la miwa pekee Kama rasilimali  kubwa katika uchumi wa nchi hiyo lakini inatoa msaada hapa nchini kwa madai ya urafiki na ujirani mwema.

Katika kuweka usawa kwa watumishi wa Umma wanaostaafu kwa kuondoa mawazo DP itaondoa kikokotoo na kufanya maboresho ya kuweka Mazingira rafiki kwa wafanyakazi.

Abduli amesema"Kwenye serikali yangu mambo ya kwanza ni kufuta kikokotoo  utafiti unaonesha kikokotoo hakipo kumsaidia mstaafu bali  kipo kumsaidi mstaafu kufa haraka".

Kwenye serikali DP itaweka mkakati wa kugeuza kikokotoo kwa watumishi waliofanya kazi ndani ya mwaka mmoja ambao hawana utovu wa maadili kwa mujibu wa taratibu zilizopo kuwakopesha nyumba kwa kukatwa kidogo kidogo kwenye mshahara wake  ili akistaafu awe na nyumba yake na atapewa fedha yake yote iliyobaki akatunze mwenyewe.

Kwa asilimia kubwa watumishi wengi wakistaafu ndipo wanakwenda kujenga huku kiwango alichopewa kuanza nacho ni kidogo hakikidhi mahitaji amesema Abdul.

Aidha amesema suala jingine atakalofanya ni kuboresha mishahara kwa watumishi waweze kuwa na morali ya uwajibikaji katika huduma wanazozitoa kwa wananchi kwa kuwa Mazingira ya kazi ni rafiki na watafanya kazi kwa starehe .

Amesema Tanzania ya Uhuru iliyoasisiwa na waasisi haifanani na Tanzania ya leo kwa sababu hivi sasa ujamaa umekwisha umebaki ubepari na ukabaila kuwepo kwa maskini na kumtaka abaki chini asinyanyuke kiuchumi huku ikirasimisha uchumi wake kwa wafanyabiasha wachache.

Serikali ya DP itafuata ndoto na nyayo za Rais wa awamu kwa kuweka usawa kwa wote na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kuwa na uzalendo utakaosaidia mzunguko wa fedha ubaki ndani kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.

Upande wa uvuvi atahakikisha anaweka utaratibu mathubuti kwa wavuvi kwa kupopeshwa  zana za uvuvi zenye viwango vinakubaliwa tofauti na ilivyo.

"Serikali kupitia wizara ya fedha inakusanya kodi bandarini za nyavu halafu wavuvi wakinunua wanafilisiwa huu ni uonevu kwa watu wa hali ya chini DP itaondoa hilo,"amesema Abdul.

Hakusita kuonesha azma ya kuwachukulia hatua viongozi watakaobainika kuhujumu mali ya Umma bila kujali nyazifa zao

Amemalizia kwa kuwasihi wananchi kuhakikisha wanashiki uchaguzi ili kupata viongozi bora na kudumisha amani.




       

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...