Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Alex Msama Amwandikia Rais Samia Waraka Huu

 


Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa,  na mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Watanzania wenzangu, Kazi na Utu?......

(Natumaini nyote mmeitikia, Tunasonga Mbele).

Mhe. Rais na Watanzania wenzangu, kwa majina ninaitwa Alex Msama Mwita.

Binafsi ni Mtanzania halisi, ninayetoka Kanda ya Ziwa, katika Mkoa wa Mara, makazi yangu ni Dar es Salaam, katika Manispaa ya Ilala, Jimbo la Uchaguzi la Ukonga, ambako nilitia nia ya kuomba nafasi ya Ubunge, ilivyo vyema ni kwamba Chama chetu kiliona wakati wangu bado, nami nilipokea kwa utiifu na unyenyekevu mkubwa maoni hayo.

Mimi Alex Msama, ni mwanachama na kada mwaminifu mwenye kiapo cha utiifu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kimaisha, mimi ni mfanyabiashara na muwekezaji wa kawaida, nikiwa Mkurugenzi wa Dira Media Group, Food Point, Msama Promotions na Msama Auction Mart.

Ninaandika waraka au barua hii ya wazi, kutoa maoni yangu binafsi, kama Ibara za 18, 21, 23 na 29 za Katiba ya Muungano wa Tanzania, zinavyoelekeza.

Mhe. Rais, nianze kwa kukupa pole nyingi kwa kazi kubwa unayoendelea nayo, kuzunguka mikoa mbalimbali hapa nchini, ukiwaelezea kwa kuwakumbusha Watanzania mambo mengi muhimu na makubwa yaliyofanywa na uongozi wako, kwa kipindi cha miaka minne na miezi kadhaa chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Sanjari na kuwaomba kura za kishindo, mnamo Oktoba 29, mwaka katika Uchaguzi Mkuu.

Mheshimiwa Rais, tangu Agosti 28, mwaka huu, zilipozinduliwa rasmi kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) pale viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe - Dar es Salaam,  nimekuwa muumini mkubwa wa kufuatilia mikutano yako yote ya kunadi sera yakinifu za CCM kwa maendeleo thabiti ya Watanzania, hakika Mhe. Rais kazi unaifanya kwa wimo wa Moyo Mkuu.

Mhe. Rais, binafsi ninaposikiliza sera za chama na mawazo yako mwenyewe juu ya mabadiliko ya kimaendeleo kwa Watanzania na ninapokutazama usoni kupitia mboni za macho yako, naiona nuru inayoangaza dhamira halisi ya wewe kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Mhe. Rais, kwa utafiti mdogo usio rasmi sana nilioufanya mimi Alex Msama, nimebaini pasina kificho kuwa matumaini makubwa ya Watanzania wameyaelekeza kwako na Serikali Imara itakayoundwa na CCM, baada ya Oktoba 29, 2025.

Aidha, Mhe. Rais, nichukue nafasi hii pia kukupongeza kwa kumaanisha kutoka katika viriba vya ndani ya moyo wangu, kwa namna ambavyo umekuwa na ngozi ngumu, moyo yabisi, fikra chanya na madhubuti kutokukatishwa tamaa na baadhi ya maneno ya hovyo kutoka kwa watu ambao wengine ni wewe umewasaidia kujipatia 'ka umaarufu' kidogo wanakotambia!

Zipo nyakati mimi Alex Msama huwa najaribu kuvaa viatu vyako nakuona ni binadamu wachache sana wenye uwezo wa kuvumilia na kustahimili upuuzi wa maneno ya kutunga unaoenezwa mitandaoni!

Mhe. Rais umetufundisha sisi Watanzania namna bora ya kukabiliana na uzushi wa watu wa hovyo, nayo ni kunyamaza na kuendelea kufanya maoinduzi kwa vitendo na kishindo cha mvumo wa radi.

Mhe. Rais unastahili pongeza za vifijo fungashi, kwa namna unavyopambana usiku na mchana kuhakikisha keki ya Taifa inawanufaisha Watanzania wote, lakini wakati huo huo watu ambao mimi nawaita vimelea, wanatumiwa na maadui wakubwa kukuvunja moyo, lakini bado upo imara na unasonga mbele, historia itakutetea kwa sentensi ndefu na kuliandika jina lako  'Dkt. Samia Suluhu Hassan', kwa WINO MPANA!

Naomba mwanao mimi Alex Msama, nikutie moyo Rais wetu, wewe ni Kiongozi mwenye maono makubwa mno.

Watanzania wengi wanajua thamani ya jasho lako katika kupambania na kupigania maendeleo yetu.

Dunia nzima imatambua uwezo wako wa kubadili yasiyowezekana kwa macho ya wengi, kuwa halisi.

Mimi Alex Msama nimebahatika kwa Neema ya Mungu kutembea maeneo mengi hapa nchini, Mhe. Rais, kazi ulizozifanya katika kuwahudumia Watanzania kwa huduma za kijamii, hazihitaji makelele na maelezo mengi, zinajitabainisha zenyewe, Watanzania ni mashahidi namba moja!

Mhe. Rais, una kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa mambo uliyoyafanya na kwa Ilani hii ya CCM iliyosheheni mambo makubwa, jina la Dkt. Samia litabaki vinywani mwa vizazi maelfu na maelfu vijavyo.

Mhe. Rais, kama Mtanzania unayo bahati ya kipekee kuliko yeyote.

Umeweka historia ya kuwa Makamu wa kwanza mwanamke, kwa kipindi cha miaka mitano na miezi mitatu.

Umeweka historia ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke kwa miaka minne na miezi kadhaa, mwanamke wa kwanza kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na sasa umeweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kupitishwa kwa kishindo na CCM kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na unakwenda kuwa Rais wa kwanza mwanamke kwa kupigiwa kura na Watanzania, wewe ni wa kipekee mno.

Mimi Alex Msama na wafanyakazi wenzangu wa Dira Media Group, Food Point, Msama Promotions na Msama Auction Mart, tunakuombea na Mungu, umalize salama siku za kampeni zilizobaki za kazi kubwa ya kukitafutia kura nyingi za kihistoria Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Watanzania tupo nyuma yako na tunaelewa nini unakifanya. Endelea kuwa imara huku ukimtumainia Mungu kwa kila hatua unayonyanyua unyayo kuipiga kwenda mbele.

Maadiko Matakatifu, kutoka katika Kitabu cha Isaya 41:10, Mungu anasema;

"Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu".

Kitabu cha Yeremia 1:8, Mungu anasema;

"Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo  pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana".

Mhe. Licha ya rekodi na historia uliyoweka kuwa mwanamke wa kwanza kushika nyazifa zote hizo, bado hauna majivuno, hauna maringo, mama hunyanyui mabega, Katika hilo Mungu akupe maisha marefu na fanaka tele.

Watanzania wenzangu, shime tuungane kwa umoja wetu kuilinda na kuipigania Amani ya nchi yetu, hii ndiyo Tunu pekee tunayojivunia katika uso wa Dunia hii.

Watu wachache kwa maslahi yao binafsi wasitupokonye Amani yetu, wakati wao wameshajitengenezea makazi huko ughaibuni.

Watanzania wenzangu, kuipoteza Amani ni jambo rahisi na jepesi sana lakini kuirejesha ni mzigo mzito wa maisha.

Tuendelee kupuuza kwa nguvu zetu zote maneno ya kutunga yanayozushwa na vimelea vyenye maslahi binafsi ya matumbo yao, tuilinde kwa wivu mkubwa Amani ya Taifa letu zuri tulilopewa na Mungu.

Nimalize waraka huu kwa kuwaomba, kuwasihi, kuwaasa na kuwakumbusha tena Watanzania wenzangu, Oktoba 29 mwaka huu, tujitokeze kwa wingi kukipigia kura kwa wingi Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atimize yale ambayo tunatamani yafanyike kwa ajili ya mstakabari wetu, kama Watanzania.

Kamwe tusikubali kucheleweshewa maendeleo tunayoyatamani na watu wachache waliojiandalia makazi yao na familia zao nje ya nchi.

Ndugu zangu Watanzania wenzangu, nitaendelea kuandika nyaraka (barua) hizi kwenu, kadiri nitakavyokuwa najaliwa ruzuku ya Oksijeni na Mwenyezi Mungu, ili kukumbushana mambo mengi muhimu yanayofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa ujumla, haya ni maoni yangu binafsi, sijaagizwa wala kuelekezwa na yeyote kuandika waraka huu.

Hii ni Salam yangu mimi Alex Msama Mwita, kwa mkono wangu mwenyewe.

Mungu awabariki sana;

Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.

Wenu katika Ujenzi wa Taifa,


Alex Msama Mwita;

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) - Dira Media Group, Food Point, Msama Promotions & Msama Auction Mart.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...