Matukio Katika Picha.
Siku ya tarehe 09.09.2025, tumeendelea na Kampeni za nyumba kwa nyumba. Kuomba kura kwa Wananchi wa Jimbo la Kawe, tukiwaomba watuamini tukawatumikie.
Mimi mgombea Ubunge jimbo la Kawe Glory Tausi nikiongozana na Mgombea U-Diwani wa Kata ya Bunju, Ndugu Suleiman Dinar, tukipita mitaa mbalimbali ya Bunju, na leo tulikua Mtaa wa Basihaya maeneo ya Chasimba.
Kampeni hizi za nyumba kwa nyumba, si tu zinatuweka karibu na Wananchi, lakini zinatupa nafasi ya kuziona Changamoto wanazokutana nazo wananchi wa maeneo haya. Mfano maeneo ya Chasimba, barabara iliyokua inapitika hapo mwanzoni kwa sasa ni mto uliokauka.
Imetolewa na:
*Glory Tausi*
*Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe*.












