Watatu wa Familia Moja Mbaroni kwa Mauaji ya Baba Mzazi

GEORGE MARATO TV
0


 Na Ada Ouko GMTV Musoma.

JESHI la polisi mkoa wa Mara linawashikilia watu watatu wa familia moja wakazi wa Mtaa Nyabisare Kata ya Bweri kwa tuhuma za mauaji ya Chacha Mwita (55) ambaye alikuwa ni Baba mzazi wa familia hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Agosti 20,2025 na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Matiku Chacha Manyengo(22), Mwajuma Chacha Nyamsiwa(45) na Manyengo Chacha Manyengo(26) ambapo walikuwa wakifanya shughuli za kilimo.

"Agosti 14,2025 Jeshi la polisi mkoa wa Mara lilipokea taarifa kutoka kwa watuhumiwa hao kuhusu kupotea kwa ndugu yao ambaye ni mume wa Mwajuma pia ni Baba mzazi wa watumiwa Matiku na Manyengo, mara baada ya kupata taarifa hiyo Jeshi la polisi mkoa wa Mara lilianza uchanguzi mara moja" Amesema Lutumo.

Katika uchunguzi wa tukio hilo Kamanda Lutumo amesema jeshi hilo lilibaini kuwa Julai 29, 2025 saa tatu asubuhi nyumbani kwa marehemu kulitokea ugomvi baina ya marehemu na mke wake, ambapo watoto wa marehemu waliingilia ugomvi huo na kuanza kumshambulia baba yao kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo chake" amesema.

Kamanda Lutumo ameleza kuwa baada ya tukio hilo watuhumiwa hao walikubaliana kuficha tukio hilo kwa kuchukua mwili wa marehemu na kuufukia katika shimo la taka lililopo pembezoni mwa nyumba yao, na kisha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wakieleza kuwa ndugu yao amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Amesema uchunguzi wa polisi uliendelea kubaini kuwa Agosti 13,2025 saa sita usiku watuhumiwa hao waliufukua mwili wa marehemu kutoka kwenye shimo la taka walipoufukia awali na kwenda kuutumbukiza ndani ya vyoo vya shule ya sekondari Nyabisare umbali wa kilomita 400 toka nyumbani kwao.

"Agosti 16,2025 jeshi la polisi mkoa wa Mara kwa kushirikiana na nyingine za kiuchunguzi walibaini na kufanikiwa kuutoa mwili wa marehemu huyo katika shimo hilo la choo wakiongozwa na watuhumiwa, Hata hivyo mwili huo ulifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi" amesema.

Aidha jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi mkoani humo na kutatua migogoro kwa kutumia vyombo vya sheria vilivyowekwa.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top