Wabunge kenya Walipiza kisasi,Waangusha Muswada Muhimu wa Serikali

GEORGE MARATO TV
0


 SIKU moja baada ya Rais wa Kenya William Ruto kudai bunge ni ngome ya ufisadi, wabunge, kwa hasira wameanza kuonyesha kucha zao kwa kuangusha miswada na maamuzi ya kisera ya Serikali Kuu.

Jumatano,Kamati ya Usalama kuhusu Bunge ilitupilia mbali Muswada wa sheria mpya ya kuongoza shughuli ya kumkabidhi mamlaka rais mpya baada ya uchaguzi.

Mswada huo uliodhaminiwa na Kiongozi wa Wengi bungeni, Kimani Ichung’wah unapendekeza Rais Mteule ateue mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Kusimamia Mpito wa Mamlaka ya Urais.

Aidha, mswada huo unapendekeza kuwa Rais mteule ateue Katibu wa kamati hiyo ya wanachama 25, tisa kati yao wakiwa wawakilishi wake.

Mswada huo pia unapanua sheria hiyo ya kuongoza shughuli ya kumpatia rais mpya afisi ili kujumuisha maafisa wengine kama Mawaziri, Mwanasheria Mkuu na Makatibu wa Wizara.

Kulingana na sheria ya sasa, Rais aliye mamlakani ndiye huonekana kuwa na usemi mkubwa katika kamati hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma.

Lakini Kamati ya Bunge kuhusu Usalama inayoongozwa na Mbunge wa Narok Magharibi Gabriel Tongoyo ilipinga mswada huo ikisema “sheria ya sasa inatosha”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top